Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,685
- 1,235
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile amewataka Wadau wa Sekta binafsi na Wadau wa usafirishaji kwa njia ya anga waliopo ndani na nje ya Nchi kuwekeza katika ununuzi wa ndege ili kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha usafiri wa anga hapa Nchini.
Mhe. David Kihenzile ametoa kauli hiyo Jijini Tanga July 30,2024 mara baada ya kutembelea kiwanda cha ndege cha Tanga ambacho ni miongoni mwa viwanja vinavyofanyiwa maboresho.
“Ombi letu kama Serikali tunawaomba Sekta binafsi watusaidie kuja kuingia kuwekeza katika Sekta ya anga, nunueni ndege za kutosha kwasababu Air Tanzania peke yake haiwezi kununua ndege kwenye viwanja vyote vilivyopo Nchini” - Mhe. David Kihenzile
Mhe. David Kihenzile Amesema ukarabati na ujenzi wa viwanja vya ndege unaoendelea hapa Nchini utakapokamilika utaongeza idadi ya Wasafiri kwenye Sekta ya anga.