Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,695
- 1,242
NAIBU WAZIRI KATIMBA AMTAKA DMO CHATO KUJITATHIMINI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amemtaka mganga mkuu na timu ya usimamizi wa shughuli za Afya wa Halmashauri(CHMT) ya Chato kujitathmini na kuhakikisha wanatoa huduma bora ya Afya kwa wananchi.
Mhe. Katimba ametoa maelekezo hayo katika mji wa Chato mkoa wa Geita kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe.Mohamed Mchengerwa kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi - CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wilayani Chato mkoa wa Geita.
Maelekezo hayo ya Mhe. Katimba ni kufuatia malalamiko yaliyoibuliwa na wananchi kuhusu mwenendo usioridhisha wa huduma za Afya.
“Nitafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha kwamba mnatimiza wajibu wenu na DMO maelekezo uyapokee na nitafuatilia kwa karibu kuona utekelezaji na tunataka wananchi wa Chato wapate huduma ya Afyayenye ubora kwasababu mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya” Amesema Mhe. Katimba