Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Anaandika Malisa
Unamkumbuka Bw.Musa Kafana, diwani wa kata ya Kiwalani (huyo aliyebebwa)? Huyu jamaa alipendekezwa kugombea unaibu meya wa jiji la Dar kupitia UKAWA. Lakini CCM wakataka kuchakachua matokeo kwa sababu kila upande ulikua na wajumbe 11, yani 11 UKAWA na 11 CCM.
So CCM wakataka kutumia nafasi hiyo kufanya udanganyifu. Lakini Mayor wa Ubungo Boniface Jacob na wajumbe wengine wa UKAWA wakapambana kiume kulinda kura. Kama mnakumbuka msimamizi wa uchaguzi huo alikua Abdalah Chaurembo (Mayor wa Temeke) ambaye alilalamika kushushiwa kipigo na Bonny na akasema atamshtaki Bonny kwa Rais (Bonny alimfundisha dawa ya urembo baada ya kutaka kuchakachua kura).
_
Wakati hayo yakiendelea mgombea ambaye ni Bw.Kafana alikuwa hoi kitandani nyumbani kwake Kiwalani. Akaenda kuletwa kwa dharura, akabebwa juujuu hadi ukumbini. Hakuweza hata kuomba kura. Mhe.Humphrey Sambo aliyefanikisha Kafana kuletwa ukumbini ndiye akamuombea kura kwa niaba. Hatimaye akashinda kwa kupata kura 12 dhidi ya Mariam Lulida wa CCM aliyepata kura 10.
Ushindi huu haukuwa rahisi, ulitafutwa kwa jasho, machozi na damu. Kuna watu walikamatwa na kuwekwa rumande siku hiyo ya uchaguzi. Kuna vijana walipigwa sana na polisi pale Karimjee kwa sababu tu ya kumshangilia Kafana. Kuna akina Bonny na Sambo waliolazimika kutumia nguvu na ubabe ili kuhakikisha haki inatendeka.
Lakini eti mtu huyohuyo leo ametangaza kujiuzulu unaibu meya, udiwani na nafasi zote ndani ya CUF na kujiunga na CCM. Kwamba anamuunga mkono JPM. Inalilah wa inalilah raajun.!