Nahitaji vifaa vinavyoweza kuchuja asali ili niweze kuipaki

kyutta

Member
Jun 11, 2016
34
25
Ndugu zangu kila siku natafuta kitu cha kufanya ili niongeze kopato nilikuwa nakwama kutokana na mazingira niliyopo, nimetamani kwenda chuo kuchukua degree ya ACC. lakini TCU wamekuja na hili la MTU mwenye DIPLOMA awe na GPA - 3.5 wakati Mimi Nina 3.3 ya Acc.
Mimi nimewaza fursa na Pesa ninayo ya kuanzia, nakaa Mkoa singida, wilaya ya Manyoni, Halmashauri ya Itigi- kwa DED LUHENDE, huku kwetu Kuna ASALI nyingi sana tena mbichi ile QUALITY kabisa ya nyuki wakubwa na wadogo, hivyo nimeona Degree siyo issue nimeamua kujikita kwenye biashara ya ASALI lakini nataka kufanya kisomi zaidi kwa kuipaki kwenye chupa ndogo, nusu Lita na Lita moja.
Sasa mahitaji yangu ni:-
1. Vifaa vya kuchujia asli (filta n.k)
2. Vifungashio(chupa) zinapatikana wapi
3. Lebal
4. Na utaratibu wa kisajili BRELLA, TFDA na TBS (ingawa sijui sana
NAOMBA MSAADA KWA MWENYE UELEWA WA HAYA MAMBO.
 
Naelewa kiasi kuhusu asali. Settler tenki zinapatikana Arusha BDTL au Chuo cha Nyuki Tabora kama utataka mawasiliano yao nijulishe.Vifungashio pia Arusha kuna kiwanda kinauza chupa za kila aina za ujazo tofauti kulingana na mahitaji yako.
 
Nami pia nahitaji kifaa hiki na vifungashi. Tafadhali naomba mawasiliano yao. Asante.
 
Naelewa kiasi kuhusu asali. Settler tenki zinapatikana Arusha BDTL au Chuo cha Nyuki Tabora kama utataka mawasiliano yao nijulishe.Vifungashio pia Arusha kuna kiwanda kinauza chupa za kila aina za ujazo tofauti kulingana na mahitaji yako.
Naomba mawasiliano yao hao BDTL mkuu.
 
kuhusu lebal mm natengeneza lebal ukiwa tayari inione pm niko dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…