Hypersonic
JF-Expert Member
- Apr 14, 2012
- 782
- 1,498
Ndugu wana bodi,
Niende moja kwa moja kwenye mada, siku ya ijumaa muda wa saa nane dakika ishirini za mchana nilipokea ujumbe kutoka airtel wakinishukuru kwa kutembelea duka lao huduma za kwa wateja na wakanitumia kumbkumbu ya kuonyesha malalamiko nilyolipoti ofisini kwao. Ili hali mimi sikuwa nimepiga simu huduma kwa wateja au kutembelea duka lolote la Airtel Tanzania.
Hili jambo likawa limenistua kidogo nikaamua kupiga huduma kwa wateja nikaongea na muhudumu wa kike ambaye sitomtaja kwa jina kwa sasa na baada ya kumweleza kuhusu suala langu akakiri kuona kuna kesi imefunguliwa kwa hiyo kumbukumbu namba niliyompatia.
Lakini akahoji tena ikiwa sijaenda ofisi yoyote lile la airtel ama kupiga simu huduma kwa wateja. Nikamjibu simu yangukwenda huduma kwa wateja tangu huu mwaka umeanza ndo hii tunayoongea mimi na wewe.
Baada ya majadiliano ya muda mfupi akaniambia nisubiri. Nilisubiri kwa muda wa dakika tano akarudi tena na kunambia samahani kwa kukuweka online kwa muda mrefu tafadhali endelea kusubiri. Baada ya dakika tatu akarudi na kunambia hawajajua kwa nini hiyo kesi imefunguliwa lakini wanaendelea kufuatilia kwa mfanyakazi aliyerekodi hiyo kesi na watanipigia kupitia namba 100.
Baada ya hapo sikupata tena simu kutoka airtel na badala yake hata ule ujumbe uliokuwa kwenye simu yangu umekuwa filtered na haupo tena. HILI NDO LIMENICHANGANYA ZAIDI.
Sijui ni nini kiko nyuma ya hili, maswali je yanaweza kuwa makosa ya kibinadamu na mhudumu anajaribu kuficha makosa yake? kama ndivyo ni kwa jinsi gani? Ikiwa kwenye maelezo yao ya awali ukipiga simu huduma kwa wateja unaambiwa simu hii inarekodiwa. Ikiwa simu zinarekodiwa manake namba zinakuwa picked automatically si ndiyo?
Kwa nini mistake kama hii itokee ? Na je ni kwa nini ule ujumbe na ile kumbukumbu namba niliyokuwa nimetumiwa viwe filtered out from inbox? Je staff wa kawaida wa kitengo cha huduma kwa wateja anaweza kuwa na access ya kuedit data kwenye system nje ya system Admin?
Wenye uelewa zaidi na hii kesi nakaribisha maoni.