mjenziwakale
JF-Expert Member
- Sep 24, 2015
- 921
- 1,390
Wakuu salama?
Aisee aiseee kimenuka tiyari hapa nyumbani kwangu kati yangu mimi na mama solomonii. Mimi ni mwanaume wa early 30's niko na mke na familia ya watoto kadhaa. Mimi siku zote huwa ni muumini wa faragha na uhuru binafsi hivyo huwa sitaki wife aguse simu yangu na wala mimi kuchokonoa simu yake, japokuwa yeye huwa ana mahaba sana na simu yangu kiasi pengine ndoto yake ni kuimiliki simu yangu na kuwa na access ya kila pahala yaani.
Sasa mimi kama ilivyo baadhi ya wanaume sijapoa sana niko na mamaz za hapa na pale mixer wa zamani wapya, wakupoozea, mwingine nimezaa Naye chobingo.
Kwa mantiki kwamba wife hana access na simu yangu hivyo huwa sifuti sms wala picha ama calls...za hizo mamaz ninazo mingle nazo siku moja moja kwamba kwa hofu ya kuja kukamatika. Sasa huyu mama kwa namna alivyo na mahaba ya dhati na hii simu sijui kafanyajefanyaje kaijua password ya simu.
Nikawa jana nimerudi zangu home saa 6 usiku nikaacha simu sebuleni nikaenda kulala. Bwana bwana kafukunyua kila kona kuanzia sms, WhatsApp, gallery mpaka koote yaani, naimiliki hii simu toka 2020 na huwa sifuti kitu chochote, kakukutana na balaa zitoo yaani Zito mno.
Ghafla naamshwa nasomewa risala juu ya tabia yangu ya umalaya kupitia ushahidi mujarabu alokutana nao kwa simu yangu, sikutaka kumsikiliza zaidi, kujibizana naye wala kujitetea maana kila kitu kiko wazi kabisa, kitu nimefanya ni kushuka kitandani kwa hasira na aibu kuu na kuelekea kulala chumba cha wageni mpaka sasa ndo nilipo najitafakari na usingizi umepaa mazima.
Hofu yangu kuu ni hatima ya hii ndoa na bila shaka imani ya huyu dada kwangu imepotea kabisaa na ni moja ya kovu kubwa sana limedevelope hapa nyumbani. Sijui tutaishije kwa kweli. Na hii pengine itampelekea kwenda kulipa kisasi, ambapo aweza ishia kujiumiza ama kuniumiza na mimi pia. Tulikuwa na amani humu ndani jamani ila ndo hivyo simu ishaniumbua.
Tafadhali wakurungwa mliowahi kulipitia hili hebu nipeni mwelekeo katika hili natokaje hapa.