Nahisi kaka yake ndiye mpenzi wa demu wangu

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
2,486
7,262
Huyu demu wangu ni mkimnya sana na muda mwingi hana time na mimi yupo busy na huyo kaka yake , wanaongea kimahaba sometime wakipigiana simu na wanajizima data kweli kweli

Pia ;:-

Sina uhakika kama kweli huyu mwanaume ni kaka yake ila wanafanana sana kwa sura hata ukiwaangalia huwezi kusema labda ni jamaa wa pembeni, ana mpost kila mara na anaandika maneno ya kimapenzi kwenye status

kila wakati anapost picha status wakiwa wametoka out pamoja na kaka yake ila cha kushangaza namuona na mtoto mdogo jinsia ya kike kama wa miaka mitatu hivi ndugu zangu

Nimepatwa na machale nimejaribu sana kumchunguza, anadai huyo ni kaka yake na mtoto ni wa kaka yake, na ukiangalia kwa makini wamefanana japo mtoto anafanana na yeye sana na anafanana pia na huyo mwanaume anaye sema ni kaka yake

Msimu huu wa mwaka mpya kampost tena wakiwa pamoja yeye na huyo anaye dai ni kaka yake wapo wamekamilika pamoja na binti yao mdogo, mbaya zaidi ameandika status i love you baby kaweka na wimbo wa mapenzi kabisa

Najiuliza sana

kama kweli ni kaka yake na anaigiza ,je kaka amekubali kufanyiwa huu mchezo mchafu na mdogo wake wa kuigiza ni wapenzi na ni mke na mume wenye katoto kadogo

Wakuu hii imekaaje maana sidhani kama hii siku ya leo huyu mwanamke ataimaliza salama
 
Fanya utafiti, ili ujihakikishie kama ni kaka ake kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…