Heroes
1.The one and only
The bold
Amenifanya niumalize mwaka vizuri, ni kama sikuishi kabisa kabla ya kufahamiana nae.
Sasa hivi ndio naishi,he give me life.
2.Edward Ngoyai Lowassa
Huyu Mzee sijui niseme nini kudhihirisha kiasi gani namkubali,nakosa maneno sahihi kabisa.
Kauli yake ya "Tulishinda lakini tukadhulumiwa,ila ushindi mkubwa zaidi ni kuvumilia kuepusha kumwaga damu za wananchi wasio na hatia"
Ishi maisha marefu my super hero E.N Lowassa
3.
Maxence Melo
Huyu kama wengi tunavyofahamu ni mwanaharakati na mpigania uhuru wa kutoa maoni.Pia muanzilishi wa JamiiForums
Kitendo chake cha kijasiri kukataa kutoa taarifa zetu sisi watumiaji wa JF kimenifanya nimkubali na kumheshimu zaidi ya hapo kabla.
Ni mfano wa kuigwa na kila mmoja.
Mungu ampe nguvu na afya njema ya kuishinda vita iliyo mbele yake...amen.
Non Heroes
1.Malaika,Mtukufu sana...
Huu ni mwaka mbaya sana kutokea kiuchumi tokea nilipokuwa na akili na kuanza kujitegemea.
Mengi na mengine mengi mengi lakini maisha magumu yanayotukabili Watanzania tulio wengi yamenifanya nimchukie sana.
Japo sikumpa kura yangu sababu sijawahi kuvutiwa na uongozi wake lakini ameshindwa kuituma nafasi ya cheo chake kunipa sababu hata moja tu ya kumkubali.
Hadi mwaka unaisha hakuna lolote alilolifanya na maana kwangu.
Huyu ni failure wa mwaka.
2.Humphrey Polepole
Huyu kaka jamani mwaka jana alitokea kuniteka sana.
Hoja zake nzitonzito zilinifanya nimfuatilie na kumkubali, ila mwaka wa 2016 kayafichua makucha yake.
Amedhihirisha rangi yake ya asili aliyoificha kutupumbaza.
Kanivunja moyo sana kama kijana niliyemtegemea kutokuongozwa na tumbo.
Najua yupo humu... "UMENIANGUSHA POLEPOLE!"
3.Naibu Spika wa Bunge Tulia
Huyu mama katutia aibu wanawake wote.
Bunge lake limekosa viwango hata vya chini kabisa.
Ametumia madaraka yake kuzima sauti za wabunge wa upinzani.
Hakuna siku aliyonikera kama alipomzuia Mh. Mbowe kumuuliza swali Waziri Mkuu Majaliwa kuhusiana na rushwa ya mil. 10 walizogaiwa wabunge wa CCM kupitisha muswada wa habari.
Nami nichukue nafasi hii kuwatakia wanachama wenzangu wote wa JF heri ya mwaka mpya.
Kila la kheri na Mungu awabarik,nawapenda wote.