Kila mmoja wetu ameshuhudia wastaafu kibao wakipewa nafasi nyeti zingine za kazi haswa katika maeneo ya wakuu wa mikoa ,.
Mtu akishataafu ni nini anatakiwa afanye katika sehemu ya umri wake uliobakia ,kuna nchi watu walistaafishwa kwa amri ya serikali ili kutoa nafasi za kazi kwa wengine na hata ikafikia kama mtu ataka kustaafu basi akiruhusiwa hata umri wa kustaafu haujafika ,na kwa kweli kuliwezekana kupatikana nafasu nyingi za kazi.
Leo TZ yenye machipukizi ya usomi ya wasomi wanaotafuta kazi ,wakikodolea macho sheemu za kazi wakipewa watu waliostaafu ,tena watu waliostaafu ni watu wenye vyeo vizito kwa maana mishahara yao monono na pensheni sio ndogo ni wa kukaa na kupumzika ,Kikwete katafutiwa kazi wamuu wa jeshi wametafutiwa kazi wote hao ni wastaafu ,Je mimi au wewe ambao tunatafuta na kungojea watu wastaafu ndio tuingie kazini kuna tamaa ikiwa wastaafu hujalizwa kwengine ?
Au nafasi zinazojazwa na wastaafu hazina mishahara hazihitaji wasomi au zinahitaji wazee wastaafu ? Kuna tatizo hapa !