Nafasi za kazi za muda za Ualimu wa TEHAMA (Part time jobs)

MANOTA ENTERPRISES

New Member
Dec 25, 2020
2
7
NAFASI ZA KAZI ZA MUDA KWA WALIMU NA WATAALAM WA TEHAMA ( PART TIME JOBS FOR TEACHERS AND ICT PERSONNELS).

HOBE E-LEARNING

Hobe E-learning ni mradi wa elimu mtandao (Electronic Learning) ambao unahusika na ufundishaji wa masomo ya sekondari kwa mfumo wa video class kwa kuzalisha video lectures kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).
Mradi huu unalenga shule za sekondari kwa masomo ya Physics, Chemistry, Biology & Geography; kidato cha 1 hadi 4.

Nafasi hizi za kazi za muda zinalenga walimu wenye uwezo wa kufundisha kwa kutumia lugha ya kiingereza kwa ufasaha kwa masomo ya Physics, Chemistry, Biology & Geography.

Sifa za jumla ni kuanzia elimu ya Diploma (stashahada) hadi Bachelor's Degree (Shahada); hata wale walimu wanafunzi (student teachers) kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa mwisho wanaweza kuomba. Pia wataalamu wa TEHAMA hasa Graphics Design, Video producers, Programmers, etc wanahitajika katika mradi huu..!!

Nafasi zinazohitajika ni zifuatazo:-

1. Walimu (Teachers); Form 1 - 4
Katika masomo ya Physics, chemistry, biology & Geography

Sifa za walimu

✓Awe na Diploma au shahada katika fani ya ualimu wa sekondari
✓Awe na uwezo wa kuongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha
✓Awe na uwezo wa kutumia computer hasa ku-type na internet
✓Awe na uwezo wa kuchora sketch/diagrams kwa masomo ya sayansi hasa biology, chemistry na physics.
✓Awe na uwezo wa kutawala darasa na kutumia muda vizuri katika ufundishaji.
✓Awe anafahamu syllabus za somo husika
✓Awe na uwezo wa kuchambua na kuandaa Notes (study notes) nzuri.

2. Graphics Designers

Sifa za mwombaji

✓Awe na uwezo au elimu katika fani ya computer kuanzia ngazi ya kidato cha 4 na kuendelea
✓Awe na uwezo wa kusoma na kuandika kiingereza kwa ufasaha.
✓Awe na uwezo wa kufanya graphics designs mbalimbali
✓Awe na uwezo wa kuandaa presentation slides (power point docs) & PDF docs
✓Awe na uwezo wa kutumia internet

3. Video producers

Sifa za mwombaji

✓Awe na uwezo wa ku-edit videos na audios
✓Awe na uwezo wa kuweka graphics kwenye audiovisual eg texts, images, animations, etc

4. Sign Artist

Sifa za mwombaji

✓Awe na uwezo wa kuchora michoro mbalimbali ya masomo ya sayansi
✓Awe na uwezo wa kusoma na kuandika kiingereza
✓Awe na uwezo wa kutumia computer

Tuma maombi kupitia sms/whatsapp 0624226549
Taja jina lako, mkoa ulipo, nafasi/somo, ngazi ya elimu na mawasiliano yako.
 
Kwa masharti mengi mliyoweka hapo, ni zaidi ya kazi ya ualimu mlipaswa mweke na mshahara ni sh ngapi.
 
Mtu akiwa na vigezo vyote hivyo, sasa kwanini aangukie katika kuajiriwa?

Hii nchi sijui tulijikwaa wapi!!!!!!
 
Hobe E-learning ni NGO au ni tuition center ya mwenge.
Kwanini pia uchukue wanafunzi wa chuo wafundishe unakwepa gharama?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom