Wakuu,
Hayawi Hayawi sasa yamekuwa!
Baada ya masiku tele kupita,
Leo nd'o naenda kutambulishwa ukweni kwa mara ya kwanza kabisa.
Nasikia ukoo mzima umekusanyika huko,
Kuanzia akina babu, bibi, baba, mama, mjomba, shangazi, mashemeji wa kike na wa kiume na ndugu wengine.
Sasa hapa najiona kama moyo Nimeuazima,
Yaani udundadunda balaa,
Akili zinazunguka,
Kichwa kinanesanesa,
Miguu inapepesuka,
Sijanywa hata chai ila najihisi nimeshiba kinoumah,
Jasho linatiririka balaa,
Mikono yote imelegea,
hadi midomo inatetema
NA
Nimevaa ile kanzu yangu matata ninayoitegemea kwenye matukio muhimu
Ila bado mwili mzima najiona kama vile nipo uchi.
----------
WAKUU,
NIPENI EXPERIENCE NA NAMNA YA KUONDOA HII HALI YA HOFU NA UOGA
KWA M'LIOWAHI KWENDA UKWENI KWA MARA YA KWANZA WAKUU!