Ndugu wana jamvi chama changu hiki kimekuwa kikivunja katiba ya nchi inayo ruhusu MTU kuwa na Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa hapa nchini.
Nafasi zingine tunagombee lakini nafasi ya uenyekiti taifa tunazuiwa eti ni ya Rais tuu. Hiki chama ni chetu wote wakulima na wafanyakazi haiwezekani tufumbwe midomo hivi.
Halafu msajili wa vyama vya siasa amekaa kimya tuu huku chama chetu hakifanyi uchaguzi. Tunalazimishwa mwenyekiti lazima awe rais. Hivi sisi wengine ndio hatuna sifa za kukiongoza hiki chama?
Naenda Dodoma kuomba fomu ya kugombea uenyekiti taifa nikinyimwa nahama hiki chama. Nimechoka kuwa msindikizaji wa wengine. Tukisema huu ni udikteta uchwara tunafukuzwa uanachama, hii sio haki bwana.