Nadhani baada ya kuikosa manati yangu ya kizungu akaja na shoka.....!!

General Galadudu

JF-Expert Member
Nov 7, 2015
1,868
2,201
Juzi alhamisi nilikuwa na wife super market tukifanya manunuzi ya hapa na pale.....sasa ktk zunguka zunguka mle ndani tukakutana na mwanamke mmoja mi nafahamiana nae lakini hawafahamiani na wife.... ki umri amenizidi kdg lakini kutokana na maisha yake kuwa ni mazuri basi hata na yeye alikuwa anajiweka vzr sana kimuonekani kiasi kwamba haikuwa rahisi hata kuamini kuwa ni mtu mzima.

A kanisalimia kwa hii mitindo ya cku hizi kukumbatiana (tena alinikumbatia kwa hisia kali) halafu akamsalimia wife kwa kumrushia tu salamu ya mbali "habari yako"tukatia story mbili tatu then tukaagana huku akisema atanitafuta ili tuongee ishu flani ya kibiashara......jambo hilo wife akalitunza moyoni.....tulipofika tu nyumbani swali la kwanza likawa ni:-yule ni nani na kwann mmekumbatiana halafu mimi akanisalimia kama vle ni mgomvi wake, aliendelea kunibana kwa maswali meeeeeeengi utadhani na yeye ni miongoni mwa wajumbe wa tume ya kuchunguza walioficha sukari.....nilitumia tu uanaume wangu kumuelewesha kwa upole na akanielewa....halafu akaja na hili tena...."nataka siku mkienda kukutana na mi niwepo ili ajue kuwa mi ni mkeo asitake kuleta dharau za kijinga" nikajua haya yote yamekuja kwa sababu za kiasili tu kwamba cku zote hawa viumbe huwa hawapendani.....

Jana sasa nikakutana na yule mama mtu mzima kwny hotel moja (lakini sikwenda na wife, maana mambo ya hawa wenzetu mengine ni ya kupuuza tu) alikuja amevaa mavazi ya balaa tupu.....yani ilikuwa akijimanua kidogo tu naona hadi maeneo yote muhimu.....nikavumilia tu......sasa cjui kuna mjinga gani aliyemwambia wife kuwa tupo pale jamani.....alikuja pale kutufanyia shambulizi moja kali na la kustukiza sana kiasi kwamba kama nisingekuwa Super General kwenye haya mambo ya kujihami kwny hizi taflani za kustukiza basi muda huu yule mwanamke asingekuwa na kiganja cha mkono wa kushoto......maana wife alikuja na shoka pale akatumia nguvu zake zote hadi zile za akiba akaisukuma kwa jazba kali sana huku akisindikizia na tusi zito ikatua juu ya meza kwa kishindo kikubwa ikiwa sentimita chache sana kutoka alipokuwa kaweka mkono wake wa kushoto.....!!nilipokuja kustuka hivi nikaona shoka iko hewani tena amelenga kumkata begani.....nikamdaka.....hakunaga jambo dogo jamani.....ile tafrani ikawa imeibua mshike mshike wa ajabu sana pale hotelini.

Asilimia kubwa ya watu wakimuunga mkono wife kwamba kanifumania huku yule mama akishindwa kabisa kutoa utetezi wowote akabaki anatetemeka tu, nilichokifanya ni kumtoa pale wife na kumpeleka nyumbani fasta halafu nikarudi kuckilizia ile kasheshe.....kwa hesabu za haraka haraka zilizopigwa na uongozi.....hasara tuliyoisababishia hotel ni kiasi cha pesa za ki Tanzania sh 467,000/

Yule mwanamke kaahidi kulipa hiyo pesa lakini akijiapiza kwamba lazima atamkomesha wife kwa kutembea na mimi......

Kwa mnaopendaga kunitupia lawama kuwa mi namkosea sana wife hata kwa hili pia nimekosea wapi jamani.....na hata yule mwanamke akiamua kunizawadia PAPUCHI na mi nikachangamkia hiyo tenda pia nitakuwa nimekosea wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…