Nyie msiojua Siasa itawachukua Miaka mingi sana kuelewa.maana hata kujifunza kwa matukio yaliyopita hamuwezi. Kubenea na Mbowe na Lowassa wanajua vizuri mchezo wa kisiasa uliochezwa hapo kulipoteza Mwanahalisi.
Endeleeni kusubiri 1+1=2 kwny Siasa. Siasa haipo direct kama Physics iliwachukua Miaka mingapi kujua kuwa Dr. Mwakyembe alitumwa na Kikwete kumsambaratisha Lowassa kupitia Richmond?
Jakaya alishatumia Bunge zaid ya mara tatu Kutikisa na kufukuza Mawaziri wake asiewataka halafu anajifanya hahusiki kukwepa lawama.
jk alikubali kusemwa sana kwny Bunge kwny Operation tokomeza lengo alipanga kumtoa NCHIMBI team lowasaa, alitumia bunge kumtoa lowassa, alitumia Bunge kumtoa Karamagi na alitumia vyombo vya habari kuwatoa Rostam na Chenge kwny uwazir wa Miundombinu. Jakaya huwa anatumia hata media hata kumtukana yeye mwenyewe kutekeleza ajenda yake.
kubenea alimtukana sana jk lakin alipomwagiwa tindikali jk alimpeleka India kwa kuwa alikuwa akifanya kazi ya kumsaidia kumsambaratisha Lowassa.
jk kaishi kwny siasa 41 years zaid ya 65%ya Umri wake ni mwanasiasa anajua kupanga karata za kisiasa vizuri sana.
kwny Siasa za Kibongo bongo Jakaya ni zaid ya Messi tena style yake ya kujifanya dhaifu dhaifu hivi ameitumia vizuri sana kupenya vikwazo na kufanikisha yake mengi