NACTE wa nini hawapokei simu za wateja wao?

KILLAKIJO

Member
Oct 12, 2014
90
11
Ndugu wana Jf

Habari za saa hizi! Nimehesabu mara 100 nikiwapikgia simu nacte kwa namba tofauti walizoweka kwenye website yao hakuna anayepokea zaidi ya mara busy mara haipokelewi kulikoni?

Ndugu wana JF lengo kuu ni kutaka kujua kwanini nilipofika kenye kipengele cha kuchagua chuo na programmes kwa ajili ya Bachelor Degree za masuala ya afya sioni chuo hata kimoja kinachotoa degree za afya?

Nina Diploma ya unesi (Diploma in Nursing) nimejisajili kupitia eneo walilotuwekea NACTE NOAS kwa Diploma Holders. Msaada wenu please kwa anayefahamu hasa watu wa nakte kama mpo.
 
Oooh my Tanzania! NACTE wameninyamazia na wadau Jf nao wameninyamanzia au hawajui kinachoendelea? I will see you when we meet face to face. Thanks a lot!
 
Ni hivi muda wa application za degree bado kuwa mvumilivu sivyo utawalaumu watu kwa haraka zako mwenyewe cha msingi jenga urafiki wa kutembelea www.nacte.go.tz haya mambo yanatangazwa hadharani kwa watz wote na sio vichochoroni
 
Hawa jamaa waligoma kupokea simu mpaka nikapiga central zone ndo wakapokea.
 
mi kuna wakat nilikua na shida na hao watu, nlichukua namba kwenye kiwebsite chao na hawakuwahi kupokea hata siku moja kwa zaidi ya wiki mbili, nlisusa
 
bado wanafanya kazi kwa mazoea. mpaka ziara ya kushtukiza ifanywe huko ndio wataamka. It's sad
 
Ni hivi muda wa application za degree bado kuwa mvumilivu sivyo utawalaumu watu kwa haraka zako mwenyewe cha msingi jenga urafiki wa kutembelea www.nacte.go.tz haya mambo yanatangazwa hadharani kwa watz wote na sio vichochoroni
Aziz Bin Adam ni website hiyohiyo ulioiataja ampapo wametutangazia diploma holders kujisajiri na kufanya admission online kuwa deadline ni 03 june 2016. Kama ingekuwa bado muda na si matangazo yao wenyewe ni ya vichochoroni je, iweje wapokee M-Pesa na kunipatia Code, ambayo nimeitumia kufanya process za admission mpaka kipengele kile cha kuchagua vyuo nikakwamia pale? Au vile vyuo vya DIT, TIA nk vilivyowekwa vikiwa na programmes za civil engineering, uhasibu na vile vya mipango na kuacha kuweka afya sio application za degree? Kama afya bado si watutangazie kwenye website zao?
 
Asanteni wote mliochangia mmenitia moyo ngoja nivute subra nisijefanya maamuzi magumu maana NACTE staff tunaishi nao kitaani!
 

Hiyo deadline ni kwa wanaotaka kusoma digrii kwenye vyuo vya ufundi, kama wewe unataka kusoma KOZI ZA AFYA kwenye vyuo vya ufundi kama vile DIT au ATC basi endelea kuhangaika na hayo ma deadline yasiyokuhusu.
Nakutakia mawasiliano mema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…