Nachukizwa na Rais wetu Magufuli kutokuhudhuria mikutano ya Wakuu wa Nchi

NgugiAchebe

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,024
688
Tukio la rais wetu kutokwenda kwenye mikutano mikubwa ya viongozi wa kuu wanachama wa Africa nahisi halitendei haki nchi yetu nashauri angalie upya msimamo wake wa kisiasa kiongozi wa nchi unapoudhuria mikutano kama hii imefanyika Rwanda unajenga uhusiano mzuri wa kidiplomasia na nchi zingine barani Africa sio kila mkutano unatuma mwakilishi, laa mkuu wetu badilika huko sio kubana matumizi tunachohitaji sisi kama wa Tanzania ni uwajibikaji na uadilifu na uzalendo katika kazi tu.

Nawasilisha wakuu
 
 
Inakusaidia nini?
 
Mkuu wa nchi kuhudhuria mikutano ni kuitangaza nchi pia. Serikali ndio yenye hela zote kwa sasa na haijengi viwanda. Bila mitaji ya nje uchumi wa viwanda ni ndoto.
 
Mkuu punguza mzuka edit vizuri post yako.
Pamoja na maoni yako lakini mimi nimemuelewa mtoa uzi. Cha msingi hapa ni kujibu hoja tatizo nini linalofanya mpaka kiongozi wetu hataki kuhudhuria mikutano ya wakuu wa nchi. Ikumbukwe kuna baadhi ya mikutano UN haitaki uwakilishi bali wanataka mwenye nyumba aje mwenyewe, sasa kama mtindo wenyewe ndio huu basi tutegemea kuna mengi muhimu kuyakosa
 


Raisi Pombe Magufuli(PhD) ni genius, anajua hiyo ni talk shop na haina manufaa yoyote yale kwa nchi yetu isipokuwa hasara tu, yeye yuko Ikulu ofisini anapitia CV za watu anaowateua kwenye nyadhifa mbali mbali!


Say no to ,,electronic African Passport"!
 
ENDELEENI KUSHANGAA KWANI VICHWA VYENU VIMEJAA MAJI. AKIENDA MWAKILISHI NA AKIENDA RAIS TOFAUTI NI IPI?

KUNA JIPYA ZAIDI YA AJENDA ZILIZOPO MBELE YA KIKAO AMBACHO AKIENDA RAIS ATAZIBADILISHA NA ASIPOENDA YEYE BASI AJENDA HAZITOJADILIWA?

TUACHE FIKIRA DHAIFU ZA KUFIKIRI KUWA RAIS AKIENDA KWENYE VIKAO VYA VIONGOZI BASI KAMA NCHI KUNA MANUFAA MAKUBWA SANA.

JIULIZENI MHE KIKWETE AMEENDA VIKAO VINGAPI NA NCHI IMENUFAIKA NA NINI KATIKA VIKAO HIVYO VYOTE ZAIDI YA 300?
 

Mikutano ya marais wa nchi za kiafrika ni ya kunywa chai na kahawa tu. Ni wachache sana wanaojali maisha duni ya wananchi wao. Kazi yao kugombea madaraka na kujitajirisha. Hata huuungano wa kisiasa wa afrika mashariki hatuuhitaji. Ni vema tubaki ni jumuiya ya kiuchumi tu kama ya nchi za ulaya vinginevyo tutaambukizana vita na fujo. Rais JPM endelea na kazi zako za kutuletea nafuu ya maisha. Wanaotaka kukuona waje kwetu.
 
HAKIKA MUNGU KAWALAANI KWA KUWANYIMA AKILI NA MAARIFA DHIDI YA MATESO YA WATZ. WANAYOYAPATA KWA KUSHINDWA KUPATA HUDUMA HATA TU ZILE ZA MSINGI ZAIDI YA MIAKA 55 YA UHURU AU TOKA KUUMBWA KWA SAYARI YA TATU HADI LEO.
HIVI UNAJUA MAANA YA KUHUDHURIA BINAFSI NA KUWAKILISHWA UMUHIMU NA UZITO WAKE AU UNATUMIA TUMBO TU KUFIKIRIA NA KUONGEA KWAKUWA UMEVIMBIWA NA BUKU 2/7 ZENU???????????????
SUALA LA KUWA NA TIJA KWA TAIFA KWA KIONGOZI KUHUDHURIA VIKAO VYA MARAIS LINATEGEMEA NA RAIS MWENYEWE UWEZO NA MSIMAMO WAKE PAMOJA NA UZALENDO WA NCHI YAKE KULILETEA MAENDELEO NA SIYO KULINGANISHA WATU MAANA MUNGU AMETUUMBA SOTE TOFAUTI.
TUNAPOKUJA KUJDAILI MASUALA YANAYOHUSU MASLAHI YA TAIFA ZIMA NA SIYO HIZO SACCOS ZENU ZA MATUMBO MTUMIE AKILI NA KICHWA.
RAIS MAGUFULI NI LAZIMA ABADILI MFUMO WAKE NA KUHUDHURIA MIKUTANO YA KIMATAIFA KWANI ANACHOKIHOFIA NINI,TUKISEMA BAJETI TUNADANGANYANA HAPA NA SISI GREAT THINKERS HATUTALIELEWA HILI ILI MRADI TU PAWEPO NA MIPANGILIO MIZURI NA PASIPO UFUJAJI WA KODI ZETU ZIKAWA MISUSED.
TUNATAKA RAIS AHUDHURIE MIKUTANO YA KIMATAIFA NA YENYE TIJA NA KULETA MANUFAA YA NCHI YETU.PERIOD!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
mkuu ahsante sana. wengi hatujishughukishi na kufikiri zaidi ya kuponda tu anachokifanya rais. Umeandika vitu vingi vya weledi. anaedhani rais akienda agdnda itabadilika na mpa pole yeye na familia yake ambayo inadhani ina mtu kumbe ina mfamo wa mtu
 
Sasa wenzie wameenda kufanya nini? au unataka kutuambia kuwa hakuna haja ya viongozi wakuu wa nchi hizi za afrika kukutana???

Kuna mtu alikuwa hahudhurii kwenye maswala ya kijamii, anatuma pesa tu, siku ya siku akafiwa na mama yake kipenzi, wananzengo nao wakamtumia michango akajikuta anatakiwa kumzika mama yake akiwa na ndugu zake tu!!!
 

Kikwete alisafiri mkamuita Vasco dagama! Leo Magufuli anatuma mwakilishi mnasema hajui kizungu-as if Kizungu kinaleta chakula mezani! Magufuli angesafiri mgemtuhumu kwamba anafuja pesa kinyume na kauli zake za kubana matumizi.....mngemshambulia kwa kutafuta hata bei ya chumba cha hoteli aliyolala! hata bei ya suti aliyovaa kwenye hiyo mikutano mngeihoji...... Binadamu hakika hatuna jema..hata ungefanyaje..lazima wenye lao wataongea tuu. Ndo maana ukitaka kufanikiwa wewe chonga mbele. Just focus!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…