Naanza kuwa na mashaka juu ya uwepo wa Mungu

David Goliath

JF-Expert Member
May 16, 2018
949
1,875
Kila nikijaribu kutafakari juu ya uwepo wa huyu anayeitwa Mungu naona kama tunapigwa, watu wengi wamekuwa wakifuata mkumbo kuamini katika hizi Imani za kidini pasipo kutumia vizuri akili Yao kwa kuhoji, na kutafakari tukianzia juu ya uwepo wa Mungu, Mungu Yuko wapi? Mungu ninani? Mbinguni ni wapi?

Uthibitisho wa kuwa Mungu yupo ni upi? Viumbe wakifa wanaenda wapi? nani aliandika vitabu vya Dini? Kwanini kama Mungu ananguvu kubwa kuliko vyote ulimwenguni ameshindwa kujitetea Hadi watu waanze kupigana jihad? Kwanini Mungu ana ubaguzi wengine wanaishi vizuri wakiwa na afya lakini wengine wanateseka na magonjwa?

Kwanini Mungu ata waangamiza binadamu Kwa moto kama ni mwenye roho ya huruma? Mungu anashindwaje kumaliza magonjwa, na majanga mengine ya kidunia, je kama wazee wetu waliokuwa hawamjui huyu Mungu tuliyeletewa na wazungu na waarabu walivyokufa Sasahivi wako mbinguni au moyotoni? Na kama wako motoni je kosa lao nilipi maana hawakuwa na taarifa yoyote kumuhusu? Kwanini huyu Mungu anatetewa na wanadamu kuwa asikosolewe Wala kuhojiwa yeye hajitokezi hadharani, Mimi Niko dilemma nahisi Bado tupo gizani juu ya haya mafundisho ya Dini, hizi sadaka na michango inayotolewa Mungu ananufaika nayo kivipi?

Nikweli ndani ya hayo majengo wanayosema ni ya Mungu yaani misikiti na makanisa yupo kweli Mungu na kama yumo mbona watu wanakaa humo na kulawiti watoto na kuiba pasipo yeye kuchukua hatua yoyote?
 
Unapoanza kuhoji uwepo wa Mungu ukiwa Umekuwa na akili timamu unaweza hata kutaipu japo haujajua vizuri kuandika Labda nikukumbushe yafuatayo:

1. Hiyo pumzi hauilipii wala haujataka kuitafuta ilikuaje pumzi ikatokea

2. Nani Huwa anakuamsha asubh unapokurupuka kwenda kwenye mishe zako? Je unaijua sekunde unayopitiwaga na usingizi na kuamka??

3. Mpaka hapo ulipo ni uwezo wako au wa wazazi wako? Usikute hata wazazi wako wanasema asingekuwa Mungu usingepatikana

4. Hao madaktari unaowakimbilia ukiumwa huo uwezo wepewa na Mungu wa kukutibu wakishindwa huwa wanasema katafute msaada wa maombi.

Mungu ameweka principle ukizifuata inaishia vizuri, hata nchi imeweka Sheria mbona majambazi wakipelekwa ndani Kwa uharifu husemi nchii hii mbaya inawatesa watu Bali unashukuru?

Ukishindwa kifuata sheria ya Mungu utaangamia, na Mungu hajaweka ziwa la moto Kwa ajili ya wanadamu bali ni kwajili yake shetani na agent zake, sasa ukitaka kumsindikiza hiyo ni hiari Yako.

Mungu hafurahii kifo cha mwenye dhambi ndio maana anakutaka ubadilishe njia zako Ili uende kule alikokuandalia ukishupaza shingo moto unakuhusu
 
Pole sana ..
Binadamu kiuasilia tumeumbwa kujua uwepo wa Mungu hata ukatae vipi lazima utakuwa hujiamini na maamuzi yako.

Mwenyezi ni mwenye hekima na ujuzi wa kila kitu ona mwanadamu mfano amepanda gari kuelekea airport kuwahi usafiri wa ndege bahati mbaya njiani akakuta bonge la foleni akaanza kulamu trafic ndege ikamuacha anakaa kidogo anapata taarifa ndege ile imepata ajali watu 50 wamefariki anaanza kifuruahi na kujiona mwenye bahati .

Anasahau kuwa mwanzo alikuwa analaumu na kuna watu 50 wameangamia halafu kwa akili zetu fupi tunataka kumkosoa Mwenyezi Mungu muumba wa mbigu na ardhi na kukadiria kila kitu ?
 
ukitaka kujua uwepo wa mungu muulize mama yako alipokea shahawa kutoka kwa konda wa daladala shahawa zikakaa tumboni zikageuka nyama baada nyama zikatoa viungo mkono mguu macho nywele ukawa binadamu ukapuliziwa roho ukaanza kupumua ukatoka huku hujijui unalia ukakua mungu akakupa riziki ya chakula na viungo kamili pumzi bure umeshiba neema zake unamkana naona sasa akili yako imekuwa kama ya baba yako konda
 
Kwa huu utafiti wangu mr david giliath anazidi kuupa marks.....

Wale mbuzi mawe waliojifanya hawauelewi uzi wamepata majibu

 
Jua kwanza ile ratiba ya jua kuchomoza na kuzama ni kama mwanga unapoanza mpka usiku kama taa ya chumbani kwako unawashwa wewe au kuzima

Je jua nan ana control is where God comes in
 
Kwa huu utafiti wangu mr david giliath anazidi kuupa marks.....

Wale mbuzi mawe waliojifanya hawauelewi uzi wamepata majibu


Mbuzi Mawe Mwenyewe bana
 
Hivi kwanini watu huwa hawadia uthibitisho wa kuwepo Mungu wakiwa bado wanaamini Mungu, kwanini huja kudai uthibitisho pale ambapo wameshaacha kuamini Mungu au wanatia mashaka kuhusu uwepo wa Mungu?

Yani uthibitisho hakikuwa ndio chenye kuwafanya waamini Mungu ila wakishakuwa wakana Mungu ndipo hutumia hoja ya uthibitisho kama sababu ya kupinga kwa uwepo wa Mungu?
 
Unapoanza kuhoji uwepo wa Mungu ukiwa Umekuwa na akili timamu unaweza hata kutaipu japo haujajua vizuri kuandika Labda nikukumbushe yafuatayo...
MWANDISHI YUKO SAWA KAHOJI VZURI TU KUHUSU UWEPO WA MUNGU WEWE UMEJIBU AS IF UNAJUA DEAR GOD ANAEXIST.ME BNAFSI NINA MASHAKA NA UWEPO WAKE BADO NAFANYA UTAFTI KUHUSU MAANDIKO YANAYOMZUNGUMZIA HUYU INVISIBLE KIUMBE.
 
Dalili moja ya uwepo wa mungu,

'Mwanaadamu kumkumbuka mungu wakati wa shida.

Nenda hospital waulize wagonjwa wale wa mda mrefu au wenye matatizo makubwa mungu yupo au hayupo halafu usikilize majibu yao.
 
MWANDISHI YUKO SAWA KAHOJI VZURI TU KUHUSU UWEPO WA MUNGU WEWE UMEJIBU AS IF UNAJUA DEAR GOD ANAEXIST.ME BNAFSI NINA MASHAKA NA UWEPO WAKE BADO NAFANYA UTAFTI KUHUSU MAANDIKO YANAYOMZUNGUMZIA HUYU INVISIBLE KIUMBE.
Wewe ni dini gani? Kama hauna dini basi endelea kuamini unachoamini
 
Back
Top Bottom