Na huyu anatambulika ni mke wa ndoa kisheria?

mr pipa

JF-Expert Member
Jul 26, 2021
2,828
5,961
Mfano umemtongoza binti ukapeleka posa mkaishi mkazaa watoto ikapita miaka 10 hamjafunga ndoa vipi huyu mwanamke atakuwa na uhalali wowote kisheria za kimahakama ikiwa hamjafunga ndoa.

Nikiwa na maana siku mkiachana anauwezo wa kudai vitu mlivyochuma kwa kipindi chote hiko ikiwa hakuna kibali chochote cha ndoa zaidi wazazi ndugu na jamii na watoto kujua nyinyi ni mke na mume?
 
Nasubiria majibu
Ila najua bila vyeti vya ndoa wanawake hupata tabu
ukikosa jibu unaongezewa swali mpaka upate jibu kwa mfano bas ikawa umeoa mwingine na ukafunga ndoa ndan ya miez hiyohiyo kumbuka wa kwanza hujafunga nae ndoa vp hapo bimkubwa anaweza kuwa uliefunga nae ndoa? Yaan yule wa pili alafu wa kwanza akawa bimdogo?
 
20240413_233250.jpg
 
Nadhani sheria za Bongo ukiishi na mwanamke zaidi ya miaka mitano huyo ni mkeo tayari
kwahy ana haki mahakaman vp ikiwa hajakuzalia na una mali za kutosha na anataka mgao na akaenda mahakaman ukasema nimemuoa miez miwil iliyopita kama vp aonyeshe ushahidi wa hiyo miaka mitano
 
Nadhani sheria za Bongo ukiishi na mwanamke zaidi ya miaka mitano huyo ni mkeo tayari
kwahy ana haki mahakaman vp ikiwa hajakuzalia na una mali za kutosha na anataka mgao na akaenda mahakaman ukasema nimemuoa miez miwil iliyopita kama vp aonyeshe ushahidi wa hiyo miaka mitano kufika au kupita?
 
Mkiishi pamoja zaidi ya miaka miwili mfululizo mnatambulika wanandoa kisheria. Lakini kama hamjafunga ndoa hapo mwanamke ili kupata mgao atatakiwa athibitishe ni kweli mlikua mnaishi kama mume na mke, hapo ndipo mwanaume unaweza kufanya ujanja janja wa kisheria na kudanganya kwamba uyo mwanamke alikua kimada tu ukifanikiwa kuishawishi mahakama utatakiwa kutoa matunzo ya watoto lakini mwanamke hatapata mgao, ila kama mmefunga ndoa mwanamke akiweka tu mezani cheti cha ndoa hapo hauna ujanja mali zinapigwa pasu kwa pasu
 
Nadhani sheria za Bongo ukiishi na mwanamke zaidi ya miaka mitano huyo ni mkeo tayari
Mkuu wanasheria wa uchochoroni wanasema ni miezi 6 (nusu mwaka). Yaani mjumbe wa nyumba kumi pamoja na majiran,i hao ndiyo mashahidi wa ndoa ya sogea tukae. Sijui kama Kuna ukweli

Maana kuna kesi imeamuliwa mwaka Jana , ya mhesh. Vicky Kamata aliyekuwa anadai mgawo wa mali za urithi za aliyekuwa mume wake Dr. Likwelilie (RIP). Vicky alikosa haki ya kupata mgawo kwa kile mahakama ilichodai kuwa ndoa ya Vicky Kamata haikusajiliwa na Rita, hivyo haitambuliki.

Yaani Vicky Kamata aliifunga ndoa kanisani na Dr. Likwelilie, lkn ndoa haikusajiliwa Rita. Mahakama ikagoma kuitambua. Vipi hizi zisizo na karatasi? Zinazotegemea kuonwa na majirani pamoja na mjumbe zotatambuliwa?
 
Mkuu wanasheria wa uchochoroni wanasema ni miezi 6 (nusu mwaka). Yaani mjumbe wa nyumba kumi pamoja na majiran,i hao ndiyo mashahidi wa ndoa ya sogea tukae. Sijui kama Kuna ukweli

Maana kuna kesi imeamuliwa mwaka Jana , ya mhesh. Vicky Kamata aliyekuwa anadai mgawo wa mali za urithi za aliyekuwa mume wake Dr. Likwelilie (RIP). Vicky alikosa haki ya kupata mgawo kwa kile mahakama ilichodai kuwa ndoa ya Vicky Kamata haikusajiliwa na Rita, hivyo haitambuliki.

Yaani Vicky Kamata aliifunga ndoa kanisani na Dr. Likwelilie, lkn ndoa haikusajiliwa Rita. Mahakama ikagoma kuitambua. Vipi hizi zisizo na karatsi? Zinaxotegemea kuonwa na majirani pamoja na mjumbe zotatambuliwa?
😂 Sogea tukae 🙌

Hv kumbe kuna kujisajili Rita.? Hii nlkuwa sijui, hv pia raia wanajua hii kitu.?
 
Kuna ndoa na pia kuna dhana ya ndoa.......

Ndoa ni ile ambayo imethibitishwa na vyetu vya ndoa........

Dhana ya ndoa inakuwa applied kwa kuishi na mwanamke kwa kipindi fulani kama wanandoa.......na hii hutumika ikiwa imethibishwa bila Shaka na mahakama na kwa ajili ya kubalance maslahi au haki za mwanamke........

Ikithibitika kuwa mwanamke kuwa mwanamke ametimiza vigezo vya dhana ya ndoa basi atahesabika kama mwanandoa na atapata stahiki zote kama mwanandoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa........

Niko tayari kusahihishwa
 
Kwahy hy sehemu ya pili inamaanisha kuwa hata kama mke ni jobless yupo ndani tuu kupika lakini mume amepambana huko amepata nyumba, gari n.k hizo pia ni mali za mke mana ni jasho lake mke 😂
Hili ni somo pana sana ndugu yangu.....tenga muda wako upitie sheria za ndoa na haki za mke wa ndoa kwenye ndoa pamoja Sheria ya dhana ya ndoa......ni somo refu lakini naamini lina manufaa makubwa sana kwako
 
Back
Top Bottom