mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,895
- 18,464
Hapa imetumika chenga ya mwili!! Kwenye taarifa moja kutolewa habari ya ongezeko la mishahara kwa asilimia 23.3 kwa kima cha chini na habari ya kupandisha mafao ya uzeeni huko PSSSF toka asilimia 25% iliyokuwa imekataliwa na waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF (waliokuwa wakipata asilimia 50%) na kuwa asilimia 33%.
Naomba ieleweke kuwa, kwa waliokuwa wanachama wa LAPF na PSPF hiki kiwango cha pensheni KIMESHUKA toka asilimia 50% kwa malipo ya mkupuo na kuwa asilimia 33%. Kiwango kimeshuka kwa asilimia 17%. Lakini kwa watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PPF na NSSF (ambao kwa sasa wote wapo PSSSF) wao mafao ya uzeeni ya mkupuo yamepanda toka asilimia 25% hadi asilimia 33% (yamepanda kwa asilimia 8%).
Naomba ifahamike kuwa mpaka sasa watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PPF na NSSF (ambao kwa sasa wote wako PSSSF) wanapostaafu hulipwa kwa asilimia 25% kwa malip[o ya mkupuo, wakati watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF (ambao kwa sasa wote wako PSSSF) wanapostaafu hulipwa kwa asilimia 50% kwa malipo ya mkupuo.
Kwa maneno mengine, mabadiliko haya yana faida kwa watumishi wa umma waliokuwa wanachama wa PPF na NSSF maana yanawapandisha "kidogo" toka 25% hadi 33%. Lakini mabadiliko haya yana hasara kwa waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF maana yanawashusha "siyo kidogo" toka 50% hadi 33%.
Nimesema ni chenga ya mwili kwa sababu watu walijadili na kusemea sana na kusifia sana kuhusu nyongeza ya mshahara hata kusahau hili la mafao ya uzeeni na kupita bila mjadala ulioshiba kwenye mitandao ya kijamii!!
Kwa upande wangu nianze na shukrani kwa Serikali yetu kwa kuondoa hii DOUBLE STANDARD iliyokuwepo kweye mafao ya uzeeni ya watumishi wa umma. Mtumishi wa umma aliyekuwa PPF au NSSF yeye aliendelea kupata mafao KIDUCHU ya asilimia 25% kwenye malipo ya mkupuo wakati watumishi wenzake wa umma waliokuwa PSPF na LAPF wakiwa wanapewa asilimia 50%. Hii tofauti ni kubwa mno! Lakini serikali ilifumbia macho jambo hili ambalo liliendeleza kuwaumiza watumishi hawa wa umma, utadhani wanatumikia serikali mbili tofauti au utadhani ni watoto wa baba tofauti!! Kwa hiyo kwa kusawazisha malipo kwa wote hilo napongeza.
Vitu vingine ambavyo huwa vinaathiri kiasi cha mapato havijaainishwa kwenye taarifa hiyo. Vitu hivyo ni:
1. Pension factor. Hii ni namba ambayo huwa inagawiwa kwenye kikokotoo cha mafao (ni denominator). Kwa kadri namba hii inavyokuwa kubwa ndivyo mafao yanavyozidi kupungua. Kwa kadri numba hii inavyokuwa ndogo ndivyo mafao yanavyozidi kuwa makubwa. Pension factor iliyokuwa inatumika PSPF na LAPF ni 580. Je hii pension factor imebaki kuwa 580 au imeongezeka au imepungua. Kama imeongezeka italamba itapunguza kiasi cha mafao! Ni vizuri wahusika wakaliweka wazi hili vinginevyo ni sawa na kuonezewa na kupunguziwa wakati huo huo na mabadiliko kutokuonekana.
2. Mshahara unaotumika kwenye kukokotoa mafao. Kwa PSPF na LAPF mshahara wa mwisho ndio ulikuwa unatumika kwenye kukokotoa mafao. Hii ina faida kwa mstaafu maana mara nyingi mshahara wa mwisho huwa ni mkubwa zaidi, hasa kama mhusika atapandishwa cheo karibu na kustaafu au serikali kuongeza mshahara. Kwa PPF na NSSF wao walikuwa wanatumia WASTANI wa mishahara "mizuri" ya miaka 3 kati ya miaka 10 ya mwisho. Hii ni mbaya sana, maana hata kama mtu atapandishiwa mshahara mwishoni, huu mshahara hautatumika kwenye kikokotoo!
Wakitafuta wastani wa mishahara wa miaka mitatu, ile miaka aliyokuwa na mshahara mdogo itameza ile aliyoongezewa kwenye kutafuta wastani. Sasa hili pia serikali lazima iliweke wazi, vinginevyo furaha ya kupandisha toka 25% hadi 33% ikawa ni furaha hewa. Lakini pia kilio cha kushuka toka 50% hadi 33% kinaweza kuwa ni kikubwa zaidi! (maana hapa kuna wanaolia waliokuwa PSPFna LAPF pia kuna wanaocheka kidogo waliokuwa PPF na NSSF).
Samahani nimelazimika kutoa andiko refu kama jitihada za kueleweka zaidi. Karibuni kwa mjadala.