Kote nchini kumekuwa na hali mbaya ya mzungunguko mdogo wa fedha mikononi mwa wananchi.
Leo asubuhi nimesikia kupitia redio Free Afrika kule Mtera wavuvi wamehama na pengine pengi tu kilio cha mzunguko mdogo wa fedha mikononi mwa wananchi.
Ikumbukwe kuwa kama kuna mzunguko mkubwa mikononi mwa wananchi hapo pia ndo Serikali inapata kodi kubwa na hivyo huduma kuwafikia wananchi.
Hata malalamiko ya Serikali kupeleka asilimia 35 ya fedha maendeleo matokeo yake ni mzunguko mdogo wa fedha na kupelekea Serikali kukosa kodi.
Kama hali hii ikiendelea basi itakuja kuigharimu sana Chama Tawala. Chukueni tahadhari mapema kama hali haijawa mbaya.