Mzungu arekodiwa akieleza jinsi wamejinga kuendelea kuididimiza Afrika

Inaumiza sana tena anaongea wazi bila kificho kwamba target Yao ni kutudidimiza....hii mikopo nayo kumbe mtego mwee...
 
Hakuna nchi inaweza kukutawala dunia ya leo, viongozi waliopo ndio wanaruhusu kutawaliwa.

Kuna tofauti kubwa sana ya mtu aliekuwa akijiamini kama Magufuli na siasa za leo za walamba miguu ya wazungu. Inasikitisha kuona kuna watu huko serikali awakumuelewa kwa kuweka tamaa zao mbele.

Ni sawa na kuacha milango ya nyumba wazi, halafu unamlaumu mwizi. Sasa hapo nani tatizo zaidi wewe au kibaka.
 
Inasikitisha ukisikiliza video hii mzungu akieleza namna ya kuididimiza Afrika Kusini mwa jangwa la sahara.

Ndiyo hao marais wetu kila siku kiguu na njia kwenda kujipendekeza ili tuendelee kuwa tegemezi, Mkwere na team yako umemsikia na kumuelewa huyo mzungu?

Leo napata kuwaelewa maRais wa Zambia Levy Mwanawasa na huyu wa sasa, Tanzania Nyerere na Magufuli

Ndiyo maana hata viongozi wetu hawataki kusikia tunaongeza tija kwenye kilimo kwwakuwa wananeemeka na misaada ya wazungu
 
Africa viongozi wetu ndio tatizo kubwa. Wao ndio wanaruhusu yote haya kwa maslahi yao binafsi. Sio kwamba hata sisi hatujui lengo la wazungu, tunajua vizuri hawataki Africa iendelee au kuelimika zaidi itakua ni tatizo kubwa.

Ila viongozi wetu wanawaendekeza tu
 
Back
Top Bottom