Ukitimua wahindi Canada unatimua labour force kubwa ambayo wameipata kwa bei rahisi.
Ukiangalia maofisini wamejaa wahindi tena wale cream.
Msimu huu wa masomo pekee wanafunzi zaidi ya 225,000 kutoka India walitakiwa kwenda Canada kwa ajili ya masomo, lakini restrictoons zilizowekwa na Canada zimepelekea Mawakala wa kutafutia wanafunzi vyuo waanze kutafutia na kuwaelekeza wanafunzi hao nchi nyingine.
Canada inatarajia kupoteza karibu US$ millioni 300+, kwa kupoteza idadi ya wanafunzi waliotakiwa ku join mwaka huu, pia, mbali ya ada, wanafunzi hao pia hutumia huduma mbalimbali nchini humo kama vile tax, vyakula, apartments n.k
Pia upande wa India itapelekea kuzidisha uhasama na uadui kati ya wahindi wa Sikh na Wahindu.
Kutoaminiani miongoni mwa Wahindi wanaoishi nchi ya India kumezidi kukua tangu Narendra Modi kuingia madarakani, kwani hata ukiangalia ndani ya Marekani kumekuwa na mwamko mkubwa sana wahindi wanaoamini katika Hindu kuungana pamoja ndani ya US na kutengeneza kitu kinaitwa Hindu Nationalism ndani ya US.
Huko India pamoja na PM Modi kukemea mara kadhaa ubaguzi wa kidini na kukanusha kujihusha nao, lakini amekua akijulikana kwa kampeni na matamshi yake kui promo Hinduism over other relogions. Imekishikanisha Chama chake na Hinduism, akasikika akinadi kuwa Hinduism siyo dini bali ni mfumo wa maisha kwa Wahindi.
Kwasasa ni kama vile Hinduization ya taifa la India imeshakamilika. Hali hii imezidi kuamsha sintofahamu kwa makundi tofauti ya kidini nchini India.