Mzoroto wa Uchumi:Asilimia kubwa ya watanzania wana msongo wa mawazo hawana furaha

Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,908
2,774
Watanzania wengi waishio mijini na vijijini wanaishi maisha duni kutokana na ukuaji wa uchumi kushindwa kugusa maisha ya watu wengi. Vijana wengi waishio mijini hawana kazi rasmi na walio na kazi kipato ni kidogo kuweza kumudu gharama za maisha. Sekta zinazokuwa kwa kasi ni mawasiliano na ujenzi ambazo kwa kiasi kikubwa hazina uhusiano wa moja kwa moja na sekta zilizoajiri mamillioni ya watanzania.

Unemployment rate ni kubwa sana Tanzania. Vijana wengi wanaomaliza chuo kikuu au vyuo vya ufundi hawapati ajira na hakuna mitaji ya kuanzisha shughuli za kuingiza kipato.

Kwa mda mrefu sana serikali imeshindwa kuzipa kipaumbele sekta za msingi kama vile viwanda na kilimo. Kukuza sekta ya viwanda itasaidia kwa kiasi kikubwa kuajiri maelfu ya vijana na kusaidia kutengeneza tabaka la kati ambalo ndio nguzo ya ukuaji uchumu sehemu yoyote ile duniani. Pia sekta ya viwanda itasaidia kukuza kilimo na hivyo kuchangamsha uchumi wa nchi na kusaidia kukua kwa service sector.

Pia, bila kudhibiti ongezeko la watu juhuzi za kupunguza umaskini zitakuwa doto. Ukuaji wa uchumi unatakiwa uwe mkubwa ukilinganisha na kasi ya ongezeko la watu…….
 
Kazi mpya ya bavicha ni kushinda kwenye mitadao ya kijamii wakilialia!!!!

Hongereni sana nyumbu kwa ubunifu wenu
 
Mbona mimi na wanao nizunguka it's a wonderful world . ..RAHA TUPU . .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…