Kwako Mzee wangu hapo magogoni uliingia kwa kasi ya ajabu sana ukijinasibu kuwa wewe ni msema kweli hivyo ukajipachika na jina lingine kuwa wewe ni mpenzi wa Mungu, hilo ni jambo zuri sana, ila mbona umekuwa na ahadi lukuki zisizotekelezeka? Kuna kundi kubwa la vijana waliositishiwa ajira Mzee wangu ukaahidi siku ya mei mosi kuwa watarudishwa kazini baada ya zoezi la uhakiki kuisha na ukasema haipiti miezi miwili, aidha ukasema pia hata watumishi waliopo kazini nao pia watapata haki yao iliyopo kwenye mikataba ya ajira ya kuongezewa mishahara yao, kuna kundi kubwa la vijana wanaokulilia Mzee, sasa hivi hata kibaba cha unga kimepanda bei Mzee tafadhali Mzee usitake laana ya watanzania waliokuamini na kukuona kama mfalme selemani yule mfalme aliyeiongoza Israel ya kale na sifa zake zikasambaa dunia nzima kwa hekima zake ikakuangukia Mzee jitahidi uendelee kuijenga heshima uliojipatia ndani na nje ya nchi kwa kuwa mkweli kama unavyosema kuwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu basi timiza falsafa yako kwa kusema kweli kama serikali haina mahitaji ya kuajiri kwa sasa uweke wazi kuwa kwa sasa kipaumbele si kuajiri, au kama haiwezekani kuwaongezea watumishi mishahara pia uweke wazi kila mtu afahamu na si kusema haizidi miezi miwili wakati tangia utoe tamko lile sasa ni takribani mwezi wa nane!!! Alamsiki.