Tulipo na tunapoelekea viongozi wastaafu ni hazina kubwa katika kushauri,kukosoa,kuehekimisha viongozi wapya na wasikivu kwa maslahi mapana ya taifa letu kimaendeleo na ustawi wake.
Siku,Wiki,Miezi na Miaka inapita na itapita lazima tukubali na tuthamini kuongozwa na marais waliopita..Wakiwa katika hatamu yapo waliotenda vema na mengine kupotoka kama ambavyo binadamu wanaweza kuwa nayo mazuri sana ama mabaya/ mapungufu.
Ni rai yangu kuona viongozi waandamizi katika serikali wakiomba kusamehewa kwa maamuzi,michakato,matendo,kauli,mitazamo,jitihada ama dira yenye kusababisha shida,taabu,mahangaiko kwa wananchi waliowapa dhamana kwa vipindi walivyoongoza.
Zipo hatua,Maamuzi,Mikakati kichama na kiserikali mlifanya kwa nia njema yamkini lakini bahati mbaya matokeo chanya mliotarajia siyo yaliopatikana au kupatikana mathalani katika falsafa ya uongozi,uchumi,siasa na mengineyo...Inawezekana kabisa mnajutia kwa namna moja au nyingine Matendo,Mawazo, maamuzi yenu,misimamo,dhana mlizokuwa nazo kwa maslahi finyu na mapana kwa taifa..Suruhisho ni kuzungumza na kujenga msingi wa kusamehewa pale mlipokosea..