Salaam,
Naheshimu sana uamuzi wa hekima wa kutong'ang'ania madaraka ya kuendelea kuongoza taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanywa na mzee wetu Dr Jakaya Kikwete..Angeliweza kabisa kutumia nguvu ya dola/Nguvu ya ushawishi kwenye chama/Kofia zake zote za kimamlaka kubadiri katiba ili kuongeza vipindi vingine vya kuongoza lakini hakuthubutu kufanya japo kauli za watu fulani fulani kutaka aendelee zilikuwapo huku na kule kama ambavyo zilikuwapo wakati wa Hayati Mwl J.K.Nyerere,Alhaji Mzee A.H.Mwinyi na Hatimae Mzee B.W.Mkapa.
Si kazi rahisi kuachia enzi kuu kama ya urais wa nchi yenye vinono vya kiuongozi japo pia ni mzigo mzito mnoo.Rais wa JMT ana mamlaka makubwa sana tena sana kikatiba yahusuyo mamlaka,nguvu na uweza wa utendaji kazi zikiwepo amri,teuzi,maelekezo,kukata majina/kupitisha majina ya wanaotakiwa ama wasiotakiwa na taifa/nchi kiuongozi n.k.Umaarufu wa Dr. Jakaya Kikwete ndani na nje ya mipaka ya JMT si wa kubezwa kuzingatia ya kuwa ni juzi juzi tu alikuwa madarakani kama raia namba moja wa taifa lenye kuinuka katika nyanja nyingi za kifulsa,rasilimali {madini,mafuta,gesi,etc} na wingi wa ukarimu kwa wawekezaji na wageni mbalimbali.
Taratibu Mh. Rais JPM ameanza kuchomoza katika shughuri za kitaifa na kiplomasia kimataifa kwa kushiriki matukio ya kitaifa katika nchi jirani kama Rwanda kisha Uganda yamkini baadae Kenya n.k n.k. Haiba ya kisiasa hujiweka wazi kwa sasa mahari wanapokutana mh. Rais JPM na Mh.Dr. Kikwete kama ambavyo imejitokeza nchini Uganda{Hekima itumike kulielewa hili}.Dr.J.Kikwete bado amekuwa na mwonekano rasmi kana kwamba bado ni rais wa JMT na hili limekuwa likijidhihirisha maeneo kadhaa anakopita ama kunena jambo lenye mguso wa kimamlaka {Mfano:Alipotembelea daraja la Nyerere,n.k}.
Kwa desturi tumeshuhudia na tulishuhudia ukimya na utulivu mkubwa ktk tamalaki ya kimamlaka pale Mzee Mwinyi alipomwachia madaraka Mzee Mkapa,Vivo hivyo Mzee Mkapa alipomwachia madaraka Mzee Kikwete.Kwamba ilifika wakati Mzee Mkapa alikataa baadhi ya miariko/Ushiriki wa matukio/n.k kuepuka kuikwadha serikali {Rais} aliepo madarakani
Nadhani Mh. JPM na Serikali yake anapaswa kupewa nafasi pana zaidi katika kutekeleza/kujiachia/kujinafasi kiuongozi na majukumu yake yakinifu kimadaraka.Hivyo ni ushauri kwa marais waliomaliza vipindi vyao,waliostaafu kuwa wakimya,watulivu,wapole,ikibidi kujichimbia mahari ambako awatavuta attention ya namna yeyote kuepusha mgongano wa nguvu/mwangwi/vigelegele vya madaraka.
Yawezekana nakashindwa kueleweka kwa baadhi ya wabobezi ktk uandishi ulionyooka,hata hivyo nina imani kubwa ujumbe wangu yawekekana umeeleweka