kiredio Jr
JF-Expert Member
- Jul 8, 2024
- 956
- 1,763
Habarini ndugu
Mimi na mzazi mwenzangu bado hatuna ndoa, ila tumebahatika kupata mtoto mmoja, kwa sasa wamerudi mkoani baada ya kuja na kukaa nyumbani kwetu kwa lengo la kumleta mtoto familia yangu imtambue.
Baada ya mtoto kufikisha miaka mitatu na nusu, nikamwambia mama yake itabidi mtoto aanze shule, na natamani mwanangu arudi Dar asome shule nzuri na ya kisasa.
Mzazi mwenzangu anadai hawezi kuruhusu hilo, ni afadhali mtoto abaki kijijini asome shule za kawaida (serikali). Nikamwambia utamsomesha wewe huko, mimi nilitaka aje Dar asome shule nzuri na tofauti na hapo sitahusika na maswala ya shule endapo atasoma tofauti na nilivyotaka.
Nadhani labda bado anachuki au kinyongo dhidi ya familia yangu, lakini hajui Elimu bora ina faida kwa mtoto na maisha yake ya baadaye, sio mimi wala yeye.
Je ni sahihi nikikataa kutoa huduma za shule endapo atasoma kijijini? Kwani lengo langu lilikuwa aje asome Dar, akae na Bibi yake (Mama yangu) na yupo tayari kwa hilo.