Mpalakugenda
JF-Expert Member
- Jun 2, 2015
- 4,326
- 4,611
Kwa waliowahi kutumia barabara ya Arusha Babati watakuwa mashahidi. Eneo mzani ulipo ni mteremkoni na kuna kona mlalo hivi.
Sijajua kulikuwa na ulazima gani umbali wa Arusha babati kuwa na vituo viwili vya mizani. Makuyuni na mdoli. Kama kuna ulazima huo, basi tanroads watafute sehemu inayostahili ila sio kwa eneo lile.
Niwaombe wataalam wanapotekeleza miradi wafanye ushirikishi hata wa taasisi nyingine ili kuangalia mdhara kwa upana wake. Naamini pale wangehusishwa jeshi la polisi idara ya usalama barabarani wasingetoa ruhusa hiyo.
Fanyeni mambo kwa weledi kulinda heshima ya elimu tunazopata.