My cup runeth over ~ Na Kikombe changu kinafurika

C. TEAM KUFURIKAA!

Mazishi ya Rasheeda yakafanyika, maana ni misiba 2 mizito wakachanganya na ya Manoa! MARINGO amelia mpaka amekuwa mwekundu! Wakazika salama, watu kibao mpaka watu wa kijijini, Maringo yupo helpless ameshikiliwa na Suzana na Evelyne, Luwi kajikaza na kakake Hachikoko lakini Maringo anagalagala, analia mbona hiki kikombe kimenifurikia namna hii hata sielewi!
Mtoto Patric Junior, ameshikiliwa na majirani wake wa kijijini

Akina Didie wakapeleka msiba Lagos wazazi hawakuja maana waliona usumbufu! Kufika kule na wanigeri unavyowajua wapo dramatic wanalia weee Richard Bank Manager nae akaenda, Musa nae akatoka Morocco akaenda rafkiake Oga tena! Alisikitika sanaaa wakazika salama wakamaliza 40 ya msiba akina Didie na Drogba wakaweka chuki zaidi kwa Wazambia wakarudi kukomesha ile deal lao in a memory of Ogadiel!


Musa akarudi kutoka Morocco Cassablanca, kaja na mrembo wa nguvu wa kizungu mixer! Mzurijee! Akaja kusalimia ndugu zake na wazazi wake akamtambulisha! Baadae akaenda ofisini kwake kwa zamani akamsalimia Bank Manager Richard akamwambia kuwa anaacha kazi amepata kazi nzuri zaidi amekonnectiwa na baba wa mke wake mtarajiwa anaomba referrence. Akaulizwa amepata bank gan akajibu HSBC Bank! Manager akachoka, bonge la international bank ukipata kazi huko maisha yako yote kama paradiso!
Akapewa reference later la nguvuu! Akashukuruuu maana sio kwa misifa ilee Bank Manager akamwambia keep in touch! Wakaagana akarudi kwa mke wake aliekuwa hotelini, asubuhi haoo wakarudi Morocco, Musa sio Mzambia tena ni Mmoroco!

Baada ya wiki 2 Patric akatoka kwa Bwana Mzee, akawa anarudi kwa Maringo, kufika anaona nyumba kimyaaaaaa! Akajua wametoka akafungua ndani viti vimewekwa pembeni haelewi kuna nini! Akaingia chumbani anamkuta Maringo amejilaza analia na mtoto yupi kwenye kitanda amelala
Akaenda akamchum kwenye shingo, Maringo ha move wala nini! Akamsogeza akamkuta anamwangalia tu! Akaanza kumwamsha anampiga mashavuni, kumcheki anapumua akajua amezimia akaja na maji anamwagia kidogo kidogo! Akashtuka! MARINGO kuangalia ni patric akajua anaota akafunga macho! Patric Akazidi kumwamsha anaendelea kummwagia maji finally Maringo akazinduka, Patric akamwambia Maringo it's me, ni mini Patric, Maringo akajibu Patric?! Akazimia jumla, Patric akambeba juu juu akampeleka hospital.
Madaktari wakamcheki maringo wakamlaza, siku 3 Patric yupo hospital na mtoto wake ambae alikuwa amekua anatambaa!
Madaktari wanashangaa huyu sio mkuu wa mkoa akawa anajikausha, mmoja akamwuliza akasema sio mimi yule ni kaka yangu tumefanana tu! Wakaamini

Finally Maringo akaamka! Kuangakia anamkuta Patric akamwuliza how?! I thot upo jela?! Wakaongea weee huku wana kiss kiss!
Maringo akamweleza kuhusu Rasheeda kuwa alijiua kabla hajajiua alimwua Baba yangu Manoa na Oga workmate wangu kwa bahati mbaya alikuwa anamlenga didie!
Patric akashtuka kusikia Didie! Akamwuliza Didie ana pacha wake?! Akajibu ndio! Akanyamaza.
Wakaongea wee baada ya siku 2 mbele wakatoka hospital kurudi home, Maringo yupo fresh wanalea watoto!
Patric akapigiwa simu, kuwa anatakiwa akatambue maiti ya mke wake mary na kuchukua custody ya watoto! Akafanya yake akarudi na watoto wake 2 na Patric jumior akawa wa 3! Maringo akaona ni a dream come true Patric kurudi ni impossible!
Patric akamwambia me nina masaa 24 tu, kukaa Zambia nahamia Norway, inabidi tuhamie wote, Maringo akaukiza kazi je?!
Patric: kaombe uhamisho wakikunyima acha kazi, kyle napoenda nimeruhusiwa kwenda na mke wangu,
Maringo akafurahi lakini hajaolewa!


MAsoud akakumbuka ahadi alioweka ya kwenda Tz na Neema akapanga safari wakaondoka kuelekea Tz, wakafika wakakutana na wazazi wa Neema Aiport, Mamake Neema amekuwa mzee sasa, mzuuuri huyooo mweupee kama zungu mama wa kitanga.
Baba yake Neema akamkumbatia akawakaribisha, wanarudi nyumbani escoted by pikipiki ya polisi wa msafara! Du! Masoyd anajionea makubwa
Wakakaribishwa na ndugu zake Neema kibao na kaka zake 3 wana familia kuubwa wakafanya sherehe pale na mchungaji akaletwa akaombea reunion! Neema akapeleka watoto wake aliozaa na late Pastor David na huyu mpya aliozaa na Masoud akamtambulisha Masoud kwake akawaeleza wazazi wake kuhusu Pastor David alivyokufa wakashangaa!
MASOUD akampa ile bahasha aliopewa na late Pastor baba yake Neema akaamini kweli David amekufa akafungua ndani akamwambia masoud isome
Masoud akaisoma! Tobaaa anashangaa akaambiwa isome kwanguvu!
Barua:
Mimi Hon.Maguspa! Namtoa mtoto wangu aolewe na David na pia naridhia kama mzazi kuishi na kufanya kazi nchini zambia mimi kama baba yake nitamlinda duniani kote
Ikatokea just incase mtoto wangu akafariki arudishwe nyumbani na hii barua mkononi aje azikiwe huku
Ikatokea mumewe akafa mtoto wangu arudhiswe nyumbani na serikali ya zambia
Ikatokea mtoto wangu akaolewa na mzambia mwingine arudi nyumbani na mtoto wangu Neema kuja kujitambulisha apate baraka zote toka kwangu mimi baba yake.
Signed na muhuri wa nchi ya Tz

Na copy ikaenda kwa waziri wa mambo ya nje ya nchi ya Zambia.
Masoyd anashangaa barua imefuata protocal kaali na yeye hajui chochote, mchungaji akaja babake neema akamwambia Pastor natala Neema na Masoud wapige magoti, Masoud very humble akapiga magoti, akawaombea baraka, moyo wake ukatulia kama baba wa Neema akasema sasa najua mwanangu regardless of religion, yupo mikononi salama, hata nikilala mauti yupo mikononi salama! Amepata mtu anayefanana na mimi kiroho, kikazi, kifikra, ana mapenzi ya kweli! Akawaombea wajukuu wote watoto wa Neema, akawaombea watoto woote wa kaka zake neema, akamwombea na mama yake sherehe ikaisha!

Wakalala Asubuhi kuamka Baba yake Neema hakuamka, amekufa!
Wakashangaa neema analia tu hajua anafanyaje, mtoto wa baba tenaa?! Hapana chezeya! Msiba mkubwa ukaweka siku 5 wakazikia makaburi ya kinondoni watu kibao, Masoud anaona tu chenga!

Drogba na Didie wakawa wanaendelea kupiga madeal ya kuoiga watu bubaa! Kiru si wakadakwa na Hidaya, Hidaya alieafuatilia non stop, akawadaka wakakimbia, wakamshinda Hidaya, wakapanda ndege ya kwenda Accra, Hidaya akajua wameenda na ya Lagos akaishia kuwakosa Airport,walipofika accra wakatoboa mpaka Lagos mojaa na hela nyiiingi saaaana wamdhulumu Mawaziri, matajiri wa Zambia, wazungu investors


ITAENDELEA SAA 6 MCHANA
 
C. TEAM KUFURIKA

Baada ya siku 7 mbele, mama mkwe wa Masoud akampa mjukuu jina la marehemu mumewe John Maguspa! Kakabatizwa na mchungaji, Masoud akaona huu ni muda wa mimi kurudi Zambia, akaaga, lakini Neema akaomba abaki amalize 40 ya baba yake akabaki na watoto Masoud akasepa

Pendo na Joseph maisha ni mazuri lakini sio mazuri saana! Maana Caroline aliumwa sana Degedege akaangukia kwenye moto akiwa camp shuleni akaungua sana akaumwa mpaka akafa, wakamzika wiki iliopita wakati Neema anamzika baba yake! Nyumba imekuwa pweke bila Caroline na Joseph nae anaumia ndani kwa ndani. Joseph akaomba uhamisho kutoka kampuni anayofanya kazi ya oil and gas kwa boss wake Masoud! Akapewa nafasi ya Dubai!, madogo wale mapacha wamekua wana miaka 2 sasa wanatembea, wakaipangisha nyumba yao na duka Pendo akaliuza kwa Suzana. Wakaondoka haoo kwenda kuanza maisha mapya in Dubai na mapacha wao

Suzana bado anaendelea grup lake ingawa Hidaya na Betty na Pendo hawapo tena wameondoka na Maringo nae amemuaga kuwa anahama nchi, akabakia na Kandi na Evelyne.
Richard akaacha kazi bank akafungua biashara yake ya restaurant, akapata wateja kibao, pembeni ya Restaurant wakafungua duka la pili la nguo,

Kandi bado anafanya kazi bank na baby wake cassandra ingawa Joe amehamishiwa kikazi johanessberg wanawasiliana kwa simu all the time

Musa alimuoa mtoto wa ki Cassablanca, anakulaje bata keshasahau all abt Mrembo na insidence ya kifo, kwa sasa wana watoto mapacha 2 wa kike wote. Musa bado anafanya kazi HSBC Bank!

Evelyne na Luwi bado wanaishi Lusaka, watoto mapacha betty and betsy wamekua hao wana miaka 2, luwi amepandishwa cheo ana hela sio kitoto, Evelyne aliacha kazi akaendeleza na kumiliki biashara za baba mkwe wake late Manoa ambazo luwi alipewa!

Patric yupo tayari kuondoka na familia yake kila kitu wamekatiwa wanasubiri saini ya Bwana Mzee,
Bwana mzee akatua wakasalimiana, akasaini contract ya Patric aondoke. Wakaingia Hidaya na Kipofu Betty! Akawauliza report vepe mmewakamata hao wa Nigeria wakajibu bado! Bwana Mzee akawaambia nawasainisha muondoke mkawatafute kwao Lagos na familia zao mtapita kwa waziri wa mambo ya nje kwanza awape msaada na mwongozo, mkiwapata muwafikishe kwa waziri wa Mambo ya nje yeye atajua jinsi ya kuongea na mimi, wakakubali ndio mkuu wakaondoka kwenda LAGOS NIGERIA! Mademu wakafurahije!

Akiwa bado anasaini form za Patric akaingia Waziri Mkuu akasalimiana na Bwana Mzee, ah Mzee Masoud umerudi?! Naona upo na kijana wako mpya Patric!

Masoud: ndio bwana namalizia malizia form aondoke ndege inaondoka baada ya masaa 3, wakaongea na waziri weee ndani ya nusu saa Patric anasubiri akampigia simu Maringo, umeshapata transfer ofisini?!

Maringo: ndio nimepata naelekea nyumbani kuwachukua watoto tuondoke

Patric: poa tukutane airport!

Masoud akamaliza mazungumzo wa waziri mkuu, akaendelea kumpa maelezo Patric! Baadae akamwambia Patric dont mess this up! Otherwise nitakurudisha jela
Patric akajibu i wont! Akaondoka zake

Patric na Maringo na watoto wao 3 wanaishi Norway!

Drogba na Didie are no where to be found! Hidaya na Betty wametafuta weee wakaamua kurudisha makambi Accra kuwatafuta!

THE END

Kwa wale ambao ni movie makers wanataka stori za kutengeneza movie tuwasiliane kwa no +255688411043 ninazO stori kibao

Kama umeipenda stori hii tuwasiliane whatsapp kwa ni +255688411043. Samahani namba hii ni ya whatsapp tuuu! Usipige Abeg!

STORI INAYOFUATA:
VALENTINE SPEACIAL: MAPENZI MUBASHARAAA ~ FOOKMI VS FOOKYU.
SAA 10 JIONI LEO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…