Mwl. Nyerere alianzisha mfumo wa vyama vingi kwa lengo la kukubali na kuonesha dunia kuwa Tanzania ina demokrasia

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
14,614
23,963
Amani kwako.

Ikumbukwe kuwa mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa na late Mwl. Nyerere ilikuwa na lengo la kukubali na kuonyesha dunia kuwa Tanzania ina demokrasia.

pic+nyerere(1).gif

Pichani: late Mwalimu Julias Kambarage Nyerere.

Siasa ina mchezo wa giza na nuru, vile vinavyofanywa gizani huwezi kuviona isipokuwa vya nuruni hapo ndipo mada imesimama.

Tukumbuke mwasisi wa uanzishwaji vyama vingi ni CCM, kupitia viongozi wake akiwepo fundi wa siasa late JKN, mzee baada ya kuambiwa na wahisani wape wananchi uhuru wa kuchagua, wakaona isiwe tabu, wakadesign na kuchambua matokeo yake ni vyama vingi ila vyama vyenyewe ni mali ya ccm.

Kuna late Kambona huyu jamaa angeweza kuwa mpinzani mahiri tatizo lake alikuwa na uroho wa madaraka mpaka alipotoka kwenye chama na kutaka kuingia msituni, tunajua kilichofuata baadaye.

IMG_20201004_072833.jpg

Pichani: late Oscah Kambona

CCM imekuwa ikiwekeza kimkakati kuonyesha wahisani kuna demokrasia ya ushindani na ndiyo maana kuna vyama vipo vipo tu havina hata mjumbe wa nyumba kumi na kila uchaguzi lazima waingize mtu kugombea urais wakijua hawapati kitu ila wanachukua fomu, mwenye uelewa unapata jibu hapo.

Wagombea urais wote waliopita dr. Wilbroud Slaa mpaka Lowassa walikuwa ni purely uccm na walikuwa kimaslahi, hivyo mfumo wa ccm uliweza kuwabeba, muite, mtulize mpe chake aondoke. Tundu Antipas Lissu siyo zao la ccm japo kakua akiongozwa na mfumo huo, ule mfumo wa muite, mtulize, mpe chake aondoke umeharibika baada ya kumchapa risasi na kushindwa kumuua, hapo ndipo shida kubwa imekuwa.


IMG_20201004_072909.jpg

Picha: Tundu Antipas Lissu.

Siasa ya vyama vingi hapa Tanzania haipo ila inakuja kuwa kweli kupitia watu kama Lissu mtu ambaye hawezi kununurika kupitia ile njia ya MMMa, sababu mojawapo inayogoma ni pale walipojaribu kumuua, upande wa wananchi wanafunguka na kufanya kweli, ila viongozi wa vyama hawana kauli thabiti pale kura zao zinapoibiwa au kubadilishwa.

Lissu ameamua kufanya mageuzi ya kweli katika mfumo usio sahihi na inaweza kuwa kweli mfumo huo ukambeba kupitia wananchi, kwa nini Mbowe as chairman nk wapo kimya au wanatoa maamuzi kimya kimya kwa mfumo wa ki_CIA hatujui!, ila jawabu mojawapo ni ile dhana ya MMMa, ambayo wapinzani wengi wamekuwa wanufaika na mpango huo wa mafao ya chukua kaa pembeni.

Njaa nayo mbaya, au ni ile dhana niliyoandika hapo juu ambayo muanzilishi wa vyama ccm anacheza unfair na tunaona wakongwe wengi wakishafanya yao, baadaye wanarejea nyumbani na kupewa kiinua mgongo kama nyadhifa kubwa kubwa wengine mabalozi, mawaziri nk, hapo ndipo unapata picha kuwa hii siasa ya vyma vingi hapa nchini ni changa la macho na Lissu anaweza kuwa asiwe yule wasiyemtegemea.


NB. Kumbukaa October ndiyo hii bado siku 24 ufanye mabadiliko na uingize historia nyingine.
 
Moderator if the topic is likely to intersect with other throgh heading read the content then make the decision to link otherwise you are undermining the intent of the presenter.
 
Back
Top Bottom