Mods, naomba kichwa kisomeke hivi, Mwinyi, kwa population hii, Tanzania lazima iendeshwe kama 'gari bovu'...
Nimejaribu kufuatilia takwimu za ukuaji wa ongezeko la idadi ya watu hapa nchini Tanzania na kingineko Duniani, nikaona kwanza ni vyema nimpongeze mwenyezi Mungu kwa kufanya kazi ngumu ya kuumba watu wote hawa kila uchao. Pia nikaona nimpongeze mwenyezi Mungu kwa kuzidisha upole maana naona kasi yake ya kuvuna walimwengu imepungua sana kiasi cha kusababisha ongezeko la idadi ya watu kwa kasi kubwa sana.
Tukirudi kwenye takwimu zetu, inaonesha kuwa wakati mwalimu Nyerere anaichukua nchi, nchi ilikuwa na idadi ya watu wanaokadiriwa kuwa milioni kumi tu, kulingana na takwimu zilizopo, na wakati Mtukuf rais Al Hassan Mwinyi anachkukua nchi, ilikuwa na idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia milioni 22.5.
Sasa nimejaribu kuangalia zama hizi za Magufuli, nchi imekuwa na idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia milioni hamsini!
Na kwa idadi hii ya watu, kuiongoza nchi sio jambo la mchezo mchezo. Some times nchi inabidi iendeshwe kama gari bovu ili tuweze kwenda.
Napenda kusema kuwa viongozi wa sasa wana kazi kubwa sana ya kuiongoza nchi ukilinganisha na zama za Mwalimu na hata zama za mzee wa ruksa.
Idadi ya watu imeongezeka sana na sasa wizara ya afya inabidi ichukue hatua stahiki kuhakikisha kuwa inadhibiti ongezeko la idadi ya watu maana huko tuendapo, hali itakuwa mbaya zaidi...
Rasilimali za nchi hii, hazitoweza kutosheleza na kukidhi mahitaji ya watu wanaozidi kuongezeka kila uchao... Just imagine, tangu nchi ipate uhuru mashamba ni yale yale, reli ya kati ni ile ile, mito ni ile ile, na tena inazidi kukauka, so rasilimali za nchi hazijaongezeka sawa na idadi ya ongezeko la watu, hali inayoashiria kuwa kadri siku zinavyozidi kusogea, uwezo wa binadamu hasa wale wanaoishi Tanzania kujipatia mahitaji yao ya msingi utakuwa mdogo zaidi. Maisha yata zidi kuwa magumu kwa sababu rasilimali zitakuwa ni za kunyang'anyana mno.
Moja ya njia za kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania, ni kudhibiti ongezeko la idadi ya watu...
Population of Tanzania, estimates according to various sorces including WB (Figures are in Millions)
Nyerere era 10-22.5
Mwinyi era 22.5- 31
Mkapa era 31- 38.8
Kikwete 38.8- 49.2
Magufuli era 49.25-50