Mwinyi: Isingekuwa katiba ningetamani Magufuli aongoze siku zote

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
IMG_3814.jpg
Rais mstafu wa awamu ya pili Tanzania, Mh Ally Hassan Mwinyi amesema kama si utawala wa Kikatiba uliopo nchini,Rais Magufuli ulipaswa kuendelea kuwa Rais wa siku zote

Mhe. Mwinyi ameyazungumza hayo jana wakati akitoa salamu za Eid El Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja , vilivyopo jijini Dar es salaam.

“Rais wetu kaleta mambo mazuri mengi sana sana, leo nchi imetulia, leo unakwenda madukani unapata huduma nzuri , leo unakwenda hospitali unaheshimiwa, leo unakwenda ofisi yoyote ile unaheshimiwa na kupata huduma nzuri,tumepata serikali nzuri ya kuwatumikia watu,” alisema Mh. Mwinyi.

“Kwahiyo kiongozi huyu ni wa kumuenzi sana sana ni wa kumsaidia sana sana na kumsifu sana na sio kusifu kwa uongo uongo, tumsifu kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa anayofanya si kwa manufaa yake bali ni kwa manufaa ya Watanzania wote. Tumuunge mkono Rais wetu, laiti isingelikuwa katiba hafupishwi muda fulani ningeshauri huyu bwana huyu awe Rais wetu wa siku zote.”

Na Emmy Mwaipopo
 
Mzee wa tathamali za semi anaomba watanzania kWA njia ya tafsida kuwa wajihadhari na raído menda kujibainisha kWA kauli ya serikali wasijejaribu kurubunika kubadili katiba ili kumuongezea muda wa kutawala. Kama ni sifa angesifiwa kWA Bajeti iliyopita kama ilitatua Matatizo ya watanzania tinge juwa anamaanisha anachokisema
 
Kwa bahati mbaya majority wameshindwa kabisa kumuelewa Mwinyi!! Wanashindwa kuelewa kwamba hata kama JPM "tutampenda" namna gani! Hata kama JPM anafanya mazuri namna gani!! Hata kama yeye Mwinyi angependa JPM atawale milele bado hilo halitawezekana kwa sababu tuna katiba iliyoweka ukomo!!
 
Mhu! Inaweza kubadilishwa wakitaka!
 
Ni Mzee Mwinyi huyuhuyu aliyepata kusema "...NCHI INA OMBWE LA UONGOZI" kabla hajaitwa IKULU au mwingine?

Mzee wa tathamali za semi anaomba watanzania kWA njia ya tafsida kuwa wajihadhari na raído menda kujibainisha kWA kauli ya serikali wasijejaribu kurubunika kubadili katiba ili kumuongezea muda wa kutawala. Kama ni sifa angesifiwa kWA Bajeti iliyopita kama ilitatua Matatizo ya watanzania tinge juwa anamaanisha anachokisema
 
Rais wetu kaleta mambo mazuri mengi sana sana, leo nchi imetulia, leo unakwenda madukani unapata huduma nzuri , leo unakwenda hospitali unaheshimiwa, leo unakwenda ofisi yoyote ile unaheshimiwa na kupata huduma nzuri,tumepata serikali nzuri ya kuwatumikia watu,” alisema Mh. Mwinyi.
Hapa mzee Mwinyi katudanganya. Hivi kwa level yake kuna ofisi ama hospitali yoyote inaweza kumdharau? Anyway, tuachane na hilo.

Kwa kevel ya mzee Mwinyi, haoni kuwa kuelezea matamanio yake hadharani ni kushawishi wananchi? DCI alipaswa kumuita kwanza mzee Mwinyi ahojiwe kabla ya Lowassa
 
Mwinyi kuongea alichokiongea ni sawa kwani yeye anashida gani wakati maslahi yake yanalindwa wakati aliuza sehemu ya nchi nani wakumgusa. Lakini hiyo ni kauli ya binadamu kama wakivyowaiga binadamu wengine ndo maana wameacha nchi iendelee kugawanyika pasipo wa kuongea. Kuna kauli aliitoa Mzee wetu Ulimwengu na Mungu azidi kumlinda popote pale alipo.Yaani tumeshindwa mazuri mpaka ya kipuuzi nayo yanatushindwa. Kuna jambo jipya ktk nchi hii ambalo raia wake Wanaweza kujifunza na maana zaidi ya mipasho na kujisifia kwa mtu binafsi. Tupo kubaya sana ila tunaongiza makuzi mwisho wake nchi ipo tu inajiendea kama vile tuko ktk kulipiza visasi kwa hivi hatutafika tunasafari ngumu sana
 
Huyu babu njaa tu hana lolote..Nchi inazidi kuharibika,hospitalini bado hali ni mbaya. Uchumi unayumba halafu anatuletea story za kitoto hapa.
 
huyu mee heshima yote na wananchi wanavyompenda anaviosha kwa maji ya betri hakuna hata jambo anasema ukweli ila yeye anataka wanawe waendelee kuwemo serikalini na mwanawe mkubwa Dr Hussein aje awe raisi wa Zanzibar njaa tu inamsumbuwa mzee wa watu utasifu mtu aliyeshindwa katika nyaja zote za kiuchumi elimu afya mawasiliano kilimo ufugaji uvuvi usafirijai dah tumsamehe bure baba yetu hajielewi
 
Back
Top Bottom