Makonde plateu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,360
- 3,317
Hili la Mwigulu na Mwalimu wake wa Shule ya Msingi (RIP Maria Mkumbo) ni Darasa la kuigwa.
Mwigulu Nchemba akiwa na Mwalimu wake wa shule ya msingi
Nimeshuhudia Mazishi ya Mwl Maria Mkumbo (RIP) ambaye ndiye alikuwa mwalimu wa Darasa la kwanza wa Dr Mwigulu Nchemba (WF). Haya nimeyajua ilipokuwa inasomwa historia ya Marehemu, nilishangazwa na kiwango cha utu alichofanya Dkt Mwigulu Nchemba kwa mwalimu wake huyo.
1) Alipougua kwa mara ya kwanza mwl Mkumbo na akagundulika kuwa na saratani alipokuwa anatibiwa KCMC, akiwa amekata tamaa, mwaka 2014, Mwigulu aliposikia akamtafutia Passport ya kusafiria Mwalimu na mtu wa kumsindikiza akampeleka Mwl wake India kwa check up na matitababu. Mwalimu alikaa miezi saba India kwa gharama za Mwigulu Nchemba kama vile ni mama yake Mzazi.
2) Mwaka 2015 Mwigulu Nchemba akampeleka tena Check UP India alipokaa takribani mwezi na mtu aliyemsindikiza kama vile ni mama yake mzazi.
3) Tangu augue 2014 Mwl Mkumbo kwa kuwa alikuwa anahudhuria clinic Ocean Road, Mwigulu aliamu kumhamishia nyumbani kwake mwalimu wake wa Shule ya Msingi tangu mwaka 2014 hadi sasa umauti ulipomkuta.
4) Yaani watoto wawili wa mwisho wa Mwigulu wamezaliwa wakamkuta Mwl wa Baba yao anaishi hapo wao walidhan tu ni bibi yao.
5) Kubwa zaidi alipougua sasa mwaka 2023 na kugundulika anatakiwa kuongezewa Damu Mwigulu akaenda na rafiki zake kumwongezea damu Mwalimu wake wa darasa la kwanza, Huu ni upendo ambao sijawahi kuuona.
6) Mwigulu aliwachukua na wajukuu waliokuwa wakiishi na Bibi yao ambaye ni mwalimu wake na kuamua kuwasomesha na kuishi nao.
7) Imenifanya nipeleleze zaidi maisha ya kiongozi huyu, nikagundua Amewachukua watoto yatima ambao wazazi wao walisoma shule moja na Mwigulu nakuwaambia kuwa yeye ni mzazi aliyebaki hivyo wasitoe chozi tena, akitolea mfano wa Meles Zenawi na rafiki zake waliopoteza maisha msituni.
8) Najua pia Kiongozi huyu ana mabweni ya watoto wenye uhitaji mbalimbali na yeye ndio amekuwa baba yao akiwepo mtoto aliyemchukua chini ya mti pale Ocean Road kwa tunaokumbuka, amemsomesha na sasa yuko kidato cha tano.
9) Nikajulishwa kiongozi huyu pamoja na majukumu ya nchi huenda mwenyewe mnadani kuwanunulia mahitaji watoto hawa na madukani kama mzazi anavyopaswa kufanya kwa watoto wake.
10) Kiongozi huyu anawatoto wengi amewasomesha na kuwalea achilia wa shule za msingi,sekondari na vyuo, wengine wako masters, Wengine PhD wengine kazini, wengine wabunge.
IMENIPA SURA NYINGINE YA MWIGULU NCHEMBA