Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,732
- 13,485
Dkt.Nchemba amesema hakuna taasisi au kampuni binafsi yoyote inaruhusiwa kukusanya kodi na mapato yote yanakusanywa na TRA na TPA, toka Kampuni ya DP World kuanza shughuli zake ufanisi umeongezeka sana, makusanyo ya bandarini nayo yamepaa hadi Trilioni 1.23 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa toka TRA ianzishwe.
Baada ya ufafanuzi huo Dkt. Nchemba alimtaka Bunge huyo kufuta kauli zake na kuomba radhi na Mpina alikiri na kufanya hivyo.
Naibu Spika, Zungu ametumia fursa hiyo kumpongeza Waziri wa Fedha kwa kutoa ufafanuzi mzuri unaoeleweka na kuwataka Mawaziri wengine kuiga mfano wake ili kudhibiti upotoshaji ndani ya Bunge.