Tunaelekea uchaguzi mkuu na joto limeishapanda sana kwa sasa. Mtihani ni mkubwa, maswali ni mengi yanataka maelezo marefu huku karatasi ya kujibia kikiwa kipande tu. Huku kuna Azimio la mgombea bila form na huku kuna No Reforms No Election. Huku wengine wakisema wao ni G55 na wengine wakiwakemea waache kuwa waasi na wapinzani wa ndani.
Lakini yote tisa je, mgombea mwenza anawaza nini? Hii nchi ambayo kwa awamu zote kadhaa tumekuwa na makamu marais wazuri lakini hawakuweza kabisa kukipata kijiti cha urais. Kwa mara ya kwanza tumeona historia ikiandika kwa namna nyingine pale ambapo rais alishinda uchaguzi akaunda serikali kisha "AKAFARIKI"
ndipo tukamuona makamu akitamalaki kiti cha uraisi.
Hii inaweza kuwa ni darasa huru na funzo kwa wanawaza wao watapataje. Huyu "Mwenza" ambaye rafu za 2015 alizochezewa Ngoyai zilimfanya atoke nje na kuongea na vyombo vya habari huku akipinga janjajanja aliyofanyiwa "Mzee wake". Baada ya miaka kumi kupita tunashuhudia "Mwenza" akiongoza kikao cha kujichagua kuwa "Mwenza"mbele ya umati bila shida.
Jicho la tai linaona mengi sana hasa yale ambayo mwewe yeye hawezi kuona. Je, tumeamua kuwa na namna nyingine ya kukipata "Kiti"? Kwamba twende tuvuke kisha tumsukume tuingie kirahisi
kama alivyoingia kirahisi. Je, "Maza" anajua hilo draft analocheza "Mwenza"? Ameishajua kuwa anamsaidia mwanaume kuketi vyema? Maana yake tunarudi kushusha bendera tena mwezi wa pili huku "Mwenza" akichekea chooni.
Kwenye mchezo wetu wa "Albastini" mwenza amelamba dume anasubiri Maza aweke jike aolewe na mechi iishe. Mwenza mtulivu huku akiona Oktoba inakaa mbali sana maana anawaza imebaki miezi michache tu afanye yake na kushika usukani.
Maza ukiweza kuelewa hii kitu basi usikubali matuta wala kona. Mwenza ameishachimba shimo refu sana maana anajua huna wa kukushauri.
Akikuponyoka tu kwisha. Kama unaenda naye kwenye mchakato basi mwezi wa pili tuna msiba tu na script imeishaandikwa ikaeje.
#MwenzaOyeeeeeee😂😂