Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,724
- 4,476
Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO), Joseph Paulo Kaheza, amepewa dhamana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita baada ya kushikiliwa kwa upelelezi kuhusu ushiriki wake katika jumuiya hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NETO tarehe 25 Februari 2025, Kaheza alikamatwa mnamo 24 Februari 2025 na baadaye kuachiwa kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea.
NETO imeishukuru jamii ya wanasheria, mashirika ya haki za binadamu kama THRDC na TLS, pamoja na vyombo vya habari na watu wote waliounga mkono juhudi za kuhakikisha kiongozi wao anaachiwa.
Aidha, NETO imesisitiza kuwa si chama cha siasa na hakihusiani na migomo yoyote, bali ni jukwaa la walimu wasio na ajira kushirikiana kupitia mitandao ya kijamii. Umoja huo umesisitiza kwamba utaendelea kuishinikiza serikali kutoa ajira kwa walimu waliomaliza mafunzo yao kati ya mwaka 2015 na 2023, kutokana na uhitaji mkubwa wa walimu mashuleni.
Soma pia: Mwenyekiti wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) Joseph Paulo anadaiwa kukamatwa na polisi mkoani Geita
"Tuna matumaini kuwa maombi yetu yatafanyiwa kazi kwa wakati," amesema Daniel Edgar Mkinga, Katibu Mkuu wa NETO, akihitimisha taarifa hiyo.
Ujumbe kutoka kwa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)