LGE2024 Mwenyekiti wa CCM Dodoma: Tukiona kiongozi wa mtaa anavimba kama harage lililopikwa baada ya kushinda, tutamuondoa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
983
2,586
Wakuu,

Inaonekana baada ya kumaliza kutishia wapinzani, wameanza kutishiana na kusimangana wenyewe ndani ya chama

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amewataka wagombea wa serikali za mitaa kuacha kujikwenza mara baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo na atakayebainika ataondolewa kwenye nafasi hiyo hata kabla ya uongozi wake kuisha.

“Wakiwa na mashati ya kijani wakati wanaombaomba hawa watu wazuri sana. Wakishapata uenyekiti, wameshajisahau chapu, mimi ni Serikali anatamba na mihuri. Safari hii ikiwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa, tukimuona mwenyekiti wa serikali ya mtaa, kijiji anavimba kama harage lililopika huyo hata katikati ya muhula tunamuondoa,” amesema Kimbisa.

==========================================================



 
Mambo imeanza kuchemka mapema,
2025 nanunua router na gunia za mahindi ya popcorn
 
harage?🤔🤔😂😂😂😂🤣🥲🤣
wazee wa hovyo hawa..🚮
 
Back
Top Bottom