DOKEZO Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Sengerema achunguzwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

monakule

Member
Sep 29, 2012
86
22
Kwa wahusika,

Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi wilaya ya Sengerema hajatoa nakala za hukumu ya kesi nyingi na leo ni siku ya 36 baada ya hukumu kutolewa, na ikumbukwe kuwa muda wa kukata rufani ni ndani ya siku 45 tu.

Hadi sasa mwenyekiti huyo hajulikani alipo na karani wake amepokea hela bila control number na ameahidi kutoa stakabadhi ya malipo siku nakala ya hukumu itakapokamilika.

Hapa maana yake kuka mchezo anacheza ambao siyo mzuri sana. Tuonaomba mamlaka za juu ziangalie hili suala kwa kina, wananchi wanaonewa sana na wanadai ni dalili za rushwa.
 
Tulia mkuu.

Muda wa kukata rufani unaanza kuhesabika pale unapopokea nakala ya hukumu.

Hakikisha nakala Yako inaonesha tarehe iliyotoka na iliyosomwa maamuzi.
 
Back
Top Bottom