Pre GE2025 Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Dorothy Semu atangaza nia ya kuwania Urais mwaka 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
1,717
4,457
Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu ametangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao.

Semu ametangaza nia hiyo leo Alhamisi Januari 16, 2025 alipokuwa akizungumza na wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akisisitiza yupo tayari kumkabili Rais Samia Suluhu Hassan wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Ndugu zangu, Tanzania inahitaji uongozi mpya utakaolinda masilahi ya Taifa na uchumi imara, jamii yenye fursa sawa, na uongozi wa uwazi. Tunaweza kubadilisha hali hii kwa kushirikiana, kuondoa changamoto hizi, na kuimarisha mustakabali wa Taifa letu.

“Niko tayari kumkabili Samia Suluhu Hassan kwenye uchaguzi wa 2025 endapo chama changu cha ACT Wazalendo kitanipa ridhaa,”
amesema Semu.


Semu.png

Source: Mwananchi
 
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, amesema

"Tanzania inahitaji uongozi mpya utakaolinda maslahi ya Taifa na uchumi imara, jamii yenye fursa sawa, na uongozi wa uwazi. Tunaweza kubadilisha hali hii kwa kushirikiana, kuondoa changamoto hizi, na kuimarisha mustakabali wa taifa letu. Niko tayari kumkabili Dkt. Samia Suluhu kwenye uchaguzi wa 2025 endapo chama changu cha ACT Wazalendo kitanipa ridhaa"

semu.jpg
 
Back
Top Bottom