Mwenyekiti wa UVCCM Moshi Vijijini Ndg Masiga Gulatone amesema anashangazwa kuona takribani miaka miwili imepita toka uchaguzi mkuu ufanyike bila ya CCM kuwachukulia hatua waliokisaliti wakati wa uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais hivyo ameomba viongozi katika ngazi zote kuanzia ngazi ya shina hadi wilaya watimize wajibu wao ili kukiacha chama katika usalama wakati huu tunapoelekea uchaguzi ndani ya chama.
"Kwa mujibu wa kanuni ya maadili na uongozi za CCM toleo la mwaka 2012 usaliti umetajwa kama kosa kubwa kuliko yote ndani ya chama lakini hapa kwetu hakuna hata mmoja amechukuliwa hatua kama vile hawakuwepo..... Tukiwabeba kwa kukaa kimya na sisi tutakuwa tunakisaliti chama chetu hivyo nawaomba viongozi wetu wachukue hatua." Alisema Masiga