DOKEZO Mwenyekiti kitongoji cha Itumbi kata ya Matundasi, Chunya aamrisha wakazi wa eneo hilo kuhama ikapo tarehe 20 Agosti 2024

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna mgogoro wa ardhi, mtaa wa Majengo mapya - jeshini, kitongoji cha Itumbi, kata ya matundasi, wilayani Chunya.

Mwenyekiti wa kitongoji anaamrisha wakazi wa eneo hilo kuhama eneo hilo ifikapo tarehe 20 Agusti 2024.

Wananchi tumejitahidi kutuma wawakilishi kuonana na mkuu wa wilaya ili kujua ukweli wa maamuzi hayo, lakini hatujafanikiwa kumuona wala kupata mawasiliano yake.

Mwenyekiti wa kitongoji anadai eneo hilo ni mali ya jeshi la JWTZ, tulipouliza maofisa wa jeshi kuhusiana na eneo hilo walituambia eneo si mali yao, na hawawezi kuhamisha watu. Isipokuwa lipo zoezi la kukagua masalia ya mabomu litakalofanywa ndani ya masaa machache.

TUNATAKA HAKI ITENDEKE KWA KUWA WANAOFUKUZWA NI WANANCHI MASKINI. MATAJIRI WALIOWEKEZA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI ENEO HILO HAWAFUKUZWI
 
Back
Top Bottom