Mwenyekiti Kikwete fanya siasa, Rais Magufuli tawala!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,137
17,908
Mwenyekiti wa CCM Taifa,Jakaya Kikwete unapaswa kufanya siasa. Unapaswa kuendelea kuwa Mwenyekiti hadi mwisho wa kipindi chako mwaka 2017. Mwaka huo,tutakusanyika hapa Dodoma kumchagua Mwenyekiti mwingine.

Rais Magufuli,tawala. Weka nchi sawa. Inyooshe. Jenga nidhamu kwenye utumishi;kusanya mapato na zuia wizi na ufisadi. Kwa kauli na matendo yako,hupendi siasa. Hutaki siasa. Vyema ukatawala na kuacha siasa kwa wanasiasa.

Mwenyekiti Kikwete,usimpe Rais uenyekiti wa chama hapo Julai 23. Mwache atawale!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 

Mbona hata sasa anafanya siasa
 
Kosa analofanya Magufuli, washauri na washabiki wake ni kudhani kuwa rais kunaenda sambamba na kuwa na nguvu za rais.
Magufuli amekuwa rais lakini amejitanabaisha kuwa maji na mafuta na upinzani na hii pekee inapunguza wigo wa nguvu za urais wake.
Ule wimbo wa kuwa na imani na Lowasa uliimbwa na walio wengi ndani ya chama.
Hawa ni watu wenye ushawishi na wapo mpaka leo na hawajawahi kumkubali Magufuli.
Ukichanganya na bajeti inayowanyonya wanyonge, sera na kauli zenye utata, ni vigumu kujua ni kundi lipi hasa linamuunga mkono Magufuli.
Labda watumishi wa umma? Jibu ni NO.
Labda ni wanafunzi wa vyuo? Jibu ni NO.
Labda ni wafanyabiashara na matajiri? Jibu ni NO.
Labda ni masikini wanaovunjiwa nyumba, walioshindwa kunywa chai, na waliogeuzwa chanzo cha kipato kwenye bajeti? Jibu ni NO.
Ni karibu kama kusema mfalme asiye na ufalme!!
 
Twende zetu magufuli wala usiangalie pembeni hakuna kutishwa wataisoma tu.
 
Mzee tupa tupa usemayo yana hekima sana, kwani watanzania lazima kuendelea kuzungumza juu ya hatima yetu huku tukichapa kazi na wala si kuchapa kazi tu bila kuifanyia tathmini ya jinsi inavyosogeza maisha yetu mbele. Kweli inaingia akilini kukubali mwongozo wa kuvuliwa baraghashia na kukataa mwongozo wa hatma ya vijana wetu? Lazima tufanye kwa karama tulizojaliwa ili taifa liende mbele, ikiwamo siasa.
 
unamawazo mgando kama mafuta ya baby care,sidhani kama umefikiri vema na kugusa kila pahala,umekurupuka kufikiri siyo?jipange tena unaweza kuandika andiko zuri zaidi ya hili,kwani hili halijashiba inavyotakiwa
 
Katika uongozi kipimo hicho kinaonyesha si mnafiki hivyo ni kiongozi mzuri
 
AKILI TATU, hebu nieleze nilipokurupuka.
Kuwa na kiongozi usiomkubali ni kazi ngumu sana.
Ni kama kuchaguliwa mke na wazee kijijini halafu unakuta hamna mnaloendana.
Nasali kila siku hii miaka mitano michungu iisha mapema.
But for the time been, WOTE TUNAISOMA!
 
Mlisema mmemchoka jk aachie uenyekiti,sasa tena mnageuka ?.


Subirini magufuli aanze kazi rasmi ya chama,mtafurahi na roho zenu
 

tatizo! usipomsifia itabidi umpinge na kumkosoa, na ukimkosoa kwa jazba unatupwa lupango, eeh,
SERKALI HII IMEKAA MSHAZARI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…