Mwenyekiti Chatanda Afungua Semina ya Viongozi wa UWT Mkoani Shinyanga, Ahimiza Wanawake Kuwania Nafasi za Uongozi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,524
1,173

MWENYEKITI CHATANDA AFUNGUA SEMINA YA VIONGOZI WA UWT MKOANI SHINYANGA, AHIMIZA WANAWAKE KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Ndg Mary Chatanda akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT Taifa, Tarehe 01.06.2024 amefungua Mafunzo ya usambazaji wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2022 Kwa viongozi na watendaji wa Makundi maalum Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga

Kongamano hilo liliandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Santiel Kirumba lililofanyika Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kutoa Mwelekeo wa CCM kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu.

Mhe. Mary Chatanda alifikisha salamu za Rais Samia Suluhu Hassan kwa wana Shinyanga kuwa anawapenda sana na kusema kuwa wahakikishe katika chaguzi zijazo wahakikishe Chama Cha Mapinduzi kinashinda kwa kishindo kwani kazi za maendeleo zimefanyika

Mhe. Chatanda ametumia adhira hiyo kuhimiza Wanawake wenye uwezo na sifa za uongozi kujitokeza kuwania uongozi Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa Kufanyika Novemba 2024 ili kujaza nafasi za Mwenyekiti wa Mtaa, Kijiji na vitongoji na wajumbe wao.

Kadharika, Mhe. Chatanda amewakumbusha Wanawake na Wananchi kujitokeza Julai 20.2024 kujiandikisha kwenye daftari la Makazi pamoja na Mpiga Kura ili kujiandaa vyema kushiriki katika uchaguzi wa serikali za Mtaa na Uchaguzi Mkuu 2025.

Mbunge Santiel amesema kuwa Kongamano hilo limejumuisha viongozi wa CCM na Serikali wakiwemo Wakurungezi wote wa Halmashauri (Shinyanga), Wabunge, Watendaji, Mama Lishe, Wajasiriamali, Waponda Kokoto, Walimu, Manesi, Maaskari, Watu wenye ulemavu.

Aidha, Mhe. Santiel Eric Kirumba amempongeza na amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha za kuwezesha kufanya Sensa ya watu na makazi.

Vilevile, Mbunge Santiel Eric Kirumba amempongeza Mama Albina Chuwa, Mkurugenzi Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na kuhakisha tunapata taarifa ya Sensa ya watu na makazi 2022/2023, hii inatusaidia kupanga Maendeleo kwa pamoja

Mwisho, Mhe. Santiel Eric Kirumba ameishukuru Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kumpa ushirikiano wa kutosha kwani Mafunzo hayo yametolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikishirikiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Santiel Eric Kirumba.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-07-02 at 19.32.48.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-02 at 19.32.48.jpeg
    188 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-07-02 at 19.32.49.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-02 at 19.32.49.jpeg
    206.8 KB · Views: 4
  • IMG-20240702-WA0020.jpg
    IMG-20240702-WA0020.jpg
    118.2 KB · Views: 4
  • IMG-20240702-WA0021.jpg
    IMG-20240702-WA0021.jpg
    77.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-07-02 at 19.32.51.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-02 at 19.32.51.jpeg
    128.9 KB · Views: 4
  • IMG-20240702-WA0016.jpg
    IMG-20240702-WA0016.jpg
    110 KB · Views: 3
  • IMG-20240702-WA0022.jpg
    IMG-20240702-WA0022.jpg
    121.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-07-02 at 19.32.50.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-02 at 19.32.50.jpeg
    114.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom