LGE2024 Mwenyekiti CHADEMA Dodoma: Maeneo ambayo yalitawaliwa na CHADEMA yalikuwa na mafanikio zaidi kuliko yalipotawaliwa na CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
296
545
Katika kuendelea na kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Dodoma Aisha Madoga amewanadi wagombea wa chama hicho katika jimbo la Kibakwe ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza wananchi kuchagua viongozi wa CHADEMA kwani sio dhaifu na hivyo kutoa wito kwao kusimamia haki zao bila kuogopa vitisho

Akiwa katika kijiji cha Iyenge jimboni humo Novemba 24. 2024 ambacho kimeongozwa na CHADEMA kwa miaka 10 ambapo amedai kuwa mafanikio makubwa yalipatikana tofauti na miaka mitano iliyopita ambayo ilitawaliwa na CCM

Soma pia: Joseph Mbilinyi: CCM hawana Maarifa, Wanavuruga Uchaguzi, Wanategemea Dola, wanateka watu na kuua watu ili kutia hofu raia


 
Back
Top Bottom