monotheist
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 790
- 1,276
Hili tatizo limemkuta kaka yangu alikua mwajiriwa wa kampuni fulani hapa jijini Dar es salaam ila kwa sasa hayupo kazini mkataba wake umeisha na amesha maliza taratibu zote za kufuatilia pesa zake NSSF na ameambiwa pesa yako tumeahatuma kwenye account yako ya bank.
Alipofika benk wakamwambia account yako imefungiwa hivyo akafanya taratibu za kurenew account yake na alikamirisha taratibu zote siku ya jumamosi 29/6/2019 na wakamwambia siku ya jumatatu tarehe 01/7/2019 tuliporudi tena wakamwambia pesa yako haijaingia kwenye account na aliporudi NSSF wakambambia arudi tena bank siku ya jumanne.
Ilipofika siku ya jumanne 02/7/2019 ambapo ni leo tulienda tawi lengine tofauti na pale tuliporenew account wakatuambia account bado haijafunguka, tulishangaa iweje tawi tuliporenew account waseme account ipo wazi lakini pesa haijaingia na tawi lingine waseme account bado haijafunguliwa.
Tukafanya maamuzi ya kwenda makao makuu ya hiyo bank kuuliza haya mambo yanakuaje tulipofika jibu ni lilelile account haijafunguliwa wakatuambia turudi tena kule tulipofungulia account.
Tulipofika wakasema ni kweli account yake haijafunguliwa ila itafunguliwa leo jioni (02/7/2019) na tutakujulisha kwa simu
Je hiki anachofanyiwa ndugu yangu ni sawa na kama si sawa tufanyeje ili aepukane na huu usumbufu ili apate haki yake maana hii pesa amuisubiri kwa muda mrefu takribani miezi 6 na ushee.