Kuelekea 2025 Mwenezi Makala: Msigwa karibu CCM, huko wanakuonea

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,538
116,426
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Amosi Makalla amemshauri aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Iringa Mjini mchungaji Peter Msigwa ahamie CCM kufuatia sakata linaloendelea baada ya Msigwa kulalamikia kutotendewa haki kwenye Uchaguzi wa Uenyekiti wa CHADEMA Nyasa uliompa ushindi Sugu.

Akiongea Mkoani Arusha leo June 03,2024, Makalla amesema “Msigwa amesema ‘najitokeza hadharani kuwaeleza Watanzania na CHADEMA sisi muda wote tumehoji Tume ya Uchaguzi kumbe sisi ni Waongo hata sisi wenyewe hatufuati taratibu za uchaguzi Mimi nimeonewa nimeibiwa kura’ sasa na Mimi namuambia Msigwa pole sana Mchungaji njoo CCM ambako kuna demokrasia tele, kuna uwazi”

“Umeonewa pole sana Mchungaji Msigwa hicho Chama hakikufai tena njoo CCM, amesema tunawadanganya tu Watu kuhusu Katiba, Tume ya Uchaguzi kumbe Chama chetu hakifuati hata sheria za uchaguzi za Chama chake”

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Mchungaji Msigwa atangaza kukata rufaa kupinga Ushindi wa Joseph Mbilinyi (Sugu) Kanda ya Nyasa

- Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa
 
Huyu jamaa ni mpuuzi sana

Screenshot_20240404-141029~2.jpg
downloadfile-3.png
 
kuna namna msigwa yeye anajua kwanini leo ccm ambao wapinzani wa chadema wana mtetea msigwa
 
Msigwa ni mrafi wa madaraka miaka 10 yote hajatosheka kukalia kiti kwamba yeye anaamini kifo tu ndio kinastahili kumuondowa kwenye uongozi vinginevyo hatakiwi kabisa kushindwa.

Msigwa anataka atuaminishe kuwa iri uwe mwanasiasa wa Kiafrica nilazima ufikiri kwa kutumia tumbo badala ya kichwa😵

Kwamba kanda yote ya nyasa msigwa anaamini wanachama wote ni mandondocha hata akosekane mtu mwenye ushawishi zaidi yake.

Kwa hili msigwa kawakosea adabu hata wanachama wenzie wa cdm kama miaka 10 hajakamili kazi aliyotakiwa kukifanyia chama chake basi huyu hafai kuwa kiongozi hata wa nyumba 10
 
Kitendo cha Msigwa kuitisha press huku vyombo karibia vyote visivyoripoti taarifa za cdm kushiriki, kunatoa jibu kuhusu uwepo wa Msigwa cdm. Ni muda mrefu Msigwa amekuwa akishutumiwa kuhamia ccm, na sasa amekosa cheo chochote ndani ya cdm, ni lazima aingie ccm rasmi.

Wakati wa Magufuli kipindi cha kuunga juhudi, Msigwa alikuwa ni mmoja ya walioshikwa mkono, ila kwa sababu kadhaa alishindwa kujiunga na ccm. Kwasasa amepata sababu ya kutekeleza azma yake. Ni vyema Msigwa akaachwa ajiunge ccm, maana akibaki cdm ataishia kuwa mletwa nongwa. Hiyo Makala alichoongea hajakiongea kwa bahati mbaya, bali anajua kinachoenda kutokea.
 
Kitendo Cha Msigwa kuitisha press huku vyombo karibia vyote visivyoripoti taarifa za cdm kushiriki, kunatoa jibu kuhusu uwepo wa Msigwa CHADEMA...
Kwa hiyo akija CCM mnampa Cheo na wanaopambania CCM wanapewa nn? Kwa hiyo ukikosa tu cheo unahama utahamia vyama vingapi?

Siamini ushawishi wa Mwenezi kama Msigwa atakubali dhambi hiyo atatubu wapi! Maana kuna wengine wameumizwa na kuteseka Kwa kumwamini.

Na aliwaaminisha kwamba chama ni Chadema leo atawaambiaje? Kwamba CCM ndiyo inafaa? Sioni akifanya hivyo.
 
Hapo ndo utanijua Nini maana CCM,Chama Dola Cha kikomonisti kiichoiva kweli kweli,ndo mana kinajiita chama DOLA,
 
Makala kajitutumua nae kaona angalau nae asikike yaani huyu buure kabisa
 
Akiongea Mkoani Arusha leo June 03,2024, Makalla amesema “Msigwa amesema ‘najitokeza hadharani kuwaeleza Watanzania na CHADEMA sisi muda wote tumehoji Tume ya Uchaguzi kumbe sisi ni Waongo hata sisi wenyewe hatufuati taratibu za uchaguzi Mimi nimeonewa nimeibiwa kura’ sasa na Mimi namuambia Msigwa pole sana Mchungaji njoo CCM ambako kuna demokrasia tele, kuna uwazi”
Mwaka huu CHADEMA imepatikana. Tabu ya CHADEMA inapofika wakati wa uchaguzi wa ndani ya chama.

Kweli demokrasia ya ndani ya chama, uongozi wa juu, wenye CHADEMA yao hawaupendi kabisa.

Msigwa komaaaa, lakini usisahau kuwa hicho chama kina wenyewe. Ama uwe toka kabila lao, au uwalambe miguu yao ndio utapata uongozi. Vinginevyo watakuwa wanakuchora tu.
 
Msigwa ni mrafi wa madaraka miaka 10 yote hajatosheka kukalia kiti kwamba yeye anaamini kifo tu ndio kinastahili kumuondowa kwenye uongozi vinginevyo hatakiwi kabisa kushindwa...
Sikilizeni hotuba ya Msigwa vizuri siku ya kukubali kushindwa alisema hakuingia chadema kutafuta cheo.Hotuba yake ilikiri kuwa yeye ni muumini wa demokrasia na kuwa alikubali kushindwa. kulikoni
 
Kwa hiyo akija CCM mnampa Cheo na wanaopambania CCM wanapewa nn? Kwa hiyo ukikosa tu cheo unahama utahamia vyama vingapi?

Siamini ushawishi wa Mwenezi kama Msigwa atakubali dhambi hiyo atatubu wapi! Maana kuna wengine wameumizwa na kuteseka Kwa kumwamini.

Na aliwaaminisha kwamba chama ni Chadema leo atawaambiaje? Kwamba CCM ndiyo inafaa? Sioni akifanya hivyo.
Akina Nassari waliwezaje hayo yote?
 
Msigwa ni mrafi wa madaraka miaka 10 yote hajatosheka kukalia kiti kwamba yeye anaamini kifo tu ndio kinastahili kumuondowa kwenye uongozi vinginevyo hatakiwi kabisa kushindwa.

Msigwa anataka atuaminishe kuwa iri uwe mwanasiasa wa Kiafrica nilazima ufikiri kwa kutumia tumbo badala ya kichwa

Kwamba kanda yote ya nyasa msigwa anaamini wanachama wote ni mandondocha hata akosekane mtu mwenye ushawishi zaidi yake.

Kwa hili msigwa kawakosea adabu hata wanachama wenzie wa cdm kama miaka 10 hajakamili kazi aliyotakiwa kukifanyia chama chake basi huyu hafai kuwa kiongozi hata wa nyumba 10

Bro nkurunzinza mbowe ana miaka mingapi kwenye uwenyekiti? Futa hii
 
Bro nkurunzinza mbowe ana miaka mingapi kwenye uwenyekiti? Futa hii
Ndio walewale walafi wa madalaka yaani wanaamini wanaongoza mandondocha na ndiomaana hawamiini katika kushindwa

Kwa mtazamo wangu kiongozi kama mbowe akipewa nchi atabadiri katiba iri tu impe uhalali wa kutawala milele. Maana tabia nikama ngozi kamwe uwezi kuibadiri
 
Back
Top Bottom