Mwanzo umri ulikuwa unaenda Taratibu (10 hadi 20) ila sasa Umri unakimbia (20 hadi 30)...

Yani kuna hali yanifkirisha,au sijui ndiyo akili za weekend...!?

Mtu kukua kutoka umri wa miaka 10 hadi 20 ilichukua mda mrefu sana.
Ila
Kukua kutoka umri wa miaka 20 hadi 30 mbona imefanyika fasta sana.
Maisha marefu ni unapozaliwa mwisho miaka 20.baada ya hapo huaamini jinsi miaka inavyokimbia,punde tu utaanza kuona mvi zinaanza kidevuni..uzee huo.
 
Hii kauli nimewahi kumsikia mzee mmoja hivi mstaafu anaisemaga. Anasema alivyofika miaka 40 alishangaa ghafla ana miaka 60. Anasema haelewi elewi kafikaje miaka 60.
Tunapoteza sana mda kwa vitu ambavyo havina maana ndomaana tunaona mda unakibia na ujaufanyia kazi za maana, wiki nzima umeenda kumuona ndugu kweli kwanini mda usikimbie
 
Back
Top Bottom