Bulelaa
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 1,137
- 2,847
Kuna jambo ambalo ni mhimu na turufu kubwa sana katika nyanja ya kiuchumi, ni pamoja na kuwa na wanasiasa wenye ushawishi mkubwa, Arusha ilishajiweka vizuri sana kwenye eneo hili, Arusha inaongoza kwa kutoa Mawaziri wakuu nchini, hii ni nzuri kwao katika kuishawishi serikali kupeleka maendeleo huko, lakini jambo lingine ni kwamba, Arusha imekuwa na wanasiasa wanaojali kwao, tofauti kabisa na ilivyo mikoa mingine kama Mwanza, Mbeya na kwingineko, Tunapokuwa tunasema, Nchi inahitaji viongozi wasomi wenye, ushawishi na wenye uchungu na maendeleo, muwe mnatuelewa, mfano mdogo, wanasiasa wa Mwanza, ni wanasiasa wanaosubiri mipango ya serikali tu tofauti na wanasiasa wa maeneo mengine ambao licha kwamba kuna mipango ya serikali, lakini bado wanakuwa ni wepesi wa kuishawishi serikali ili iingize mipango inayotokana na nguvu ya ushawishi na iliyosahaulika katika kupanua wigo wa naendelea katika eneo husika
Wanasiasa, ni kiungo mhimu sana katika kushawishi serikali ili ipelekee maendeleo, Yaani utakuta jiji la mwanza, licha ya kuwa na ukaribu wa ziwa Victoria, kuna maeneo hayana maji! Huu ni uzembe wa viongozi na siyo serikali, maji hayo hayo ya Victoria yamefika Dodoma ilihali yanapoanzia, hayajaenezwa, Wana Mwanza, timueni wote wabunge mlionao, hao ndiyo wanaochangia Mwanza iwe ya hovyo
Ikumbukwe, Jiji la Mwanza, na Jiji la Arusha, watu wake wanakawaida ya kushindana kimaendeleo, jambo ambalo ni la kuigwa, ni zuri na linafaa, hii inamaanisha kwamba, hamuwezi kuwa mnachagua viongozi legelege ili hali mnapenda jiji lenu liwe juu
Sifahamu agenda ya mkoa wa Mwanza kukatwa na kuzaliwa Geita ilitoka kwa nani, usikute pia ni siasa na ushawishi wa mkoa shindani wenu waliwazidi mbinu, bila kufahamu madhala ya badaye, mkaona ni sawa tu, Mwanza kijiografia ni ndogo kuliko Tabora, Dodoma, Morogoro n.k, lakini mikoa hiyo haikugawanywa mpaka leo
Hii maana yake nini,??
Nikirudi kwenye mada
Mkoa wa mwanza, kwa siku za usoni, utapitwa na kila mkoa kiuchumi kwa sababu mapato mengi ambayo yalikuwa yakiuinua mkoa huo na kushika nafasi ya pili kitaifa katika kuliingizia Taifa mapato yake, mengi yapo katika mkoa mpya wa Geita iliyokuwa wilaya ya Mkoa huo
Sioni ajabu mkoa wa Mwanza kwa sasa kushushwa nafasi yake na mikoa kama Njombe, Kilimanjaro, Arusha n.k kwa sababu imebaki na sifa moja tu ya milima milima yenye mawe
Ukija kwenye Ziwa, hata Geita ziwa lipo, na hata hivyo, Ziwa hili kwa nyakati tofauti limekuwa likiendeshwa kisiasa tupu
Wana Mwanza kufurahia kuzalisha mkoa mpya wa Geita huku wakisahau sehemu kubwa ya maeneo yote ya mkoa wa Mwanza, haina resources zozote zaidi ya ziwa ambalo nalo samaki zilishapungua, kunaifanya Mwanza iwe ni mji usiochangamka mbeleni
Ingawa kwa upande mwingine kwa serikali ni kusogeza huduma na miundombini kwa haraka kwa wananchi katika mikoa mipya, hata hivyo, Ukweli unapembuka kwamba, mwisho wa tambo za wana Mwanza kuwa ndilo jiji ambalo huchangia pakubwa zaidi kimapato ya serikali umewadia