MWANZA: Mtu Mwingine auawa kwa kukatwa mapanga usiku Sengerema

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Wakati upelelezi wa tukio la watu saba wa familia moja kuuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana ukiendelea, mauaji mengine ya aina hiyo yametokea wilayani Sengerema.

Safari hii, mkazi wa Kijiji cha Bilulumo, Kata ya Kafunzo, James Mgambo (71) aliuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Kafunzo, Dotto Bulunda, mke wa Mgambo aliyetajwa kwa jjina la Nyangalo Masisa (65) alijeruhiwa katika tukio hilo na amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Sengerema.
“Chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana na polisi wamefika kwa ajili ya uchunguzi,” alisema Bulunda.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bilulumo, Said Makelemo alisema mapanga mawili yanayoaminika kutumika yalikutwa eneo la tukio.

Mmoja wa majirani wa familia hiyo, Lameck Kasabulilo alisema hawakusikia kelele za kuomba msaada.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Hakimu Elisha, mazishi ya Mgambo yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya ukoo yaliyopo kijijni hapo.

Mgaga Mkuu wa Hospitali Teule Wilaya ya Sengerema, Dk Mary Jose alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti, huku hali ya majeruhi ikiendelea vizuri.

Mkuu wa Wilaya Sengerema, Zainab Telack alisema tayari uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo umeanza na kuapa wahusika watasakwa na kutiwa mbaroni.
 
Usishangae kuambiwa sababu kubwa ni ushirikina! Mara mauaji ya albino! huko nako polisi wanatakiwa waanzishe ''Kanda maalum'' ya kipolisi ili kukomesha aina hii ya mauaji ya kiholela pasipo kusahau pia utolewaji wa elimu stahiki.
 
Kwa wenzetu ukizeeka unaenziwa na kupewa kipaumbele kwenye mambo mengi tu ya kijamii. Bongo ukizeeka, hasa kanda ya ziwa mapanga yanakuhusu!. Inahuzunisha sana.
 
Huo mkoa ni wa kufanyia maombi maalum, kwa nini hawana huruma wala ubinadamu? Mauaji ya mapanga? Inassikitisha sana, ukiwa na mzazi mzee Mwanza ufanye mchakato wa kuwahamisha mkoa.
 
Angekuwa mwanasiasa ingeletwa story ingine.
Hapo muone asili ya hiyo kanda kuuwana kwa mapanga ni kawaida yao sana hata kwa visa vya kipuuzi.
Nimeishi huko nimeshuhudia mauaji ya kinyama kila wakati .
 
Mwanza na Kanda ya Ziwa Kwa ujumla imani za kishirikiana zimetawala sana. Mauaji mengi ni ya kulipizana kisasi. Hata mtu akifariki kwa kifo cha kawaida lazima waende kwa waganga. Huko wanatoka na jina la mtu nao wanakuja kumua huyo alitajwa. Ndugu wa aliyeuwa nao kama wanaubavu wanaua Familia iliyomuua ndugu yao hivyo kufanya mzunguko usioisha wa mauaji ya kulipiza kiasi.
Wana Mwanza na Watanzania Kwa ujumla ileleweke kifo ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Kila mmoja lazima atakufa. Kwa mtu akifa hakuna sababu ya kumkatia rufaa kwamba kifo chake hakikuwa cha haki. Kama kungekuwa na rufaa hiyo mwenyekuisikiliza angekuwa ni Mungu. Mbona basi tunatoa hukumu ya hiyo rufaa sisi wanaadamu!?
 
Umejuaje?
 
Looh, inabidi nikamchukue bibi yangu huko nyakalilo, sengerema maana ana macho mekundu wasukuma hawachelewi kufyaranga mapanga kisa macho ya uzeeni hayana afya kwa sababu ya moshi wa mabua.
 
ukiwangali wapole saana watu wa mwanza unajiuliza haya mauaji wanayafanyaje mbona wana nyuso za kondoo saana wanaonekana wakarimu, au kuna wageni toka nchi jirani huja kufanya hili tukio?
 
Kutwa nzima wanakesha humu kuwasema wanaume wa dar wanashindwa kwenda kusaidiana na ndugu zao huko,au hata hawa hapa mjini nao walishafanya yao huko?
 
Looh, inabidi nikamchukue bibi yangu huko nyakalilo, sengerema maana ana macho mekundu wasukuma hawachelewi kufyaranga mapanga kisa macho ya uzeeni hayana afya kwa sababu ya moshi wa mabua.

hahahahaha...imebidi nicheke tu. na bibi yangu wa kule Busekeseke na mwingine Nyehunge na wale wa Isaka na Kishinda inabidi niwatafutie utaratibu wa kuwahamisha
 
Nilileta uzi miaka ya nyuma kuwaasa wasukuma wezagu kuwa hii tabia inatuharibia sofa yetu ya upole kwa sababu ya imani za kishirikina lkn wengi waliniandama sana wakitaja mikoa mingine. Ukweli waasisi wa mauaji ya mapanga ni usukumani baada ya kuwaamini sana waganga wa jadi ambao 89% ni mataperi na waogo.
 
ukiwangali wapole saana watu wa mwanza unajiuliza haya mauaji wanayafanyaje mbona wana nyuso za kondoo saana wanaonekana wakarimu, au kuna wageni toka nchi jirani huja kufanya hili tukio?
Ngoja kwanza nilale kesho takupatia jibu lililochambuliwa kwa undani hasa uelewe chanzo chake na namna unavyoweza kuwanasa wakata mapanga kirahisi kama kweli serikali ina nia ya dhati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…