Awamu hii si ruhusa kukosoa/kutoa maoni yako hasi dhidi ya watawala. Mnatakiwa kuimba mapambio tu kwa watawala ili tusalimike.View attachment 366236
Mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Frank Sanga na mwandishi wake, Elias Msuya wameitwa na polisi kuhojiwa kuhusu makala iliyochapishwa na gazeti hilo kuhusu utendaji wa jeshi hilo.
Wakati Msuya alipigiwa simu jana na kuhojiwa leo asubuhi kuhusu makala aliyoandika, Sanga ameitwa leo na tayari ameondoka ofisini kwake kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kuitikia wito huo.
Makala hiyo ya uchambuzi yenye kichwa cha habari “Polisi na Hofu ya Watawala Kuondoka Madarakani”, ilichapishwa na gazeti hilo jana.
Chanzo: Mwananchi
Ukweli unauma sana.Serikali baada ya MADAWATI itayarishe na kujenga magereza,maana kwa mwendo huu nusu ya watanzania watmalizikia huko.
Baadhi yetu hatukubaliani na wewe...kauli yako hapa ni ya uchochezi...ni aina ya watu ambao mnaleta hoja halafu yakitokea mnaingia mitini...ni uongo kusema nusu ya watanzania watamalizikia kwenye magereza, hii ni kauli ya uchochezi na isiyo na ukweli wowote...umekuwa 'alarmist' kwa issues ambazo ni za kawaida...sasa hivi naanza kuisoma makala hiyo, ili name nione ni kwa vipi imefanya hao Ndugu zetu waitwe na polisi, lakini ni 'uongo' kuanza kubashiri kuwa nusu ya watanzania wataishia magerezani..